Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 108 2025-04-22

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuiongezea bajeti TARURA kutoka shilingi bilioni 275.03 katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 hadi shilingi bilioni 886.30 Mwaka wa Fedha 2024/2025. Barabara ya Mkuyuni – Mahina – Nyakato, yenye urefu wa kilometa 11.02 imeshafanyiwa usanifu wa kina, ambapo makadirio ya kuijenga kwa tabaka la lami ni shilingi bilioni 22. Ujenzi wa barabara hiyo kwa urefu wa kilomita mbili unatarajiwa kuanza Mwaka wa Fedha 2025/2026. (Makofi)