Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 1

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba nipate majibu ya maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; barabara hii, takribani miaka minne sasa, nimekuwa nikiiomba Serikali iweze kufanyiwa kazi. Ninawashukuru kwa kukamilisha usanifu, ili barabara iweze kuanza kazi, lakini barabara hii ni mbaya sana. Ninatamani nyongeza ya fedha za Serikali zinapopatikana, basi zi-reflect kwenye kile tunachokiuliza kila wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ninamwomba sasa Mheshimiwa Waziri, kwa sababu ameshatoa ahadi nyingi na Serikali imeshatoa ahadi nyingi kuhusu barabara hii, ambayo kiukweli imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Nyamagana, Mheshimiwa Waziri yuko tayari sasa pengine akajionee hiki ninachokisema kwa macho na waweze kuchukua hatua haraka kabla hatujafika huko tunakokwenda? Ninakushukuru sana. (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Stanslaus Mabula, ambaye kwa kweli, amekuwa akipaza sauti yake kusemea wananchi wake wa Jimbo la Nyamagana kuhusiana na kupata barabara nzuri na barabara hizi za TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mimi na yeye tutakaa, tutakubaliana na tutapanga ratiba, kwa ajili ya kwenda kufika katika eneo la barabara hii ili kujionea hali halisi. Ninaomba nimhakikishie kwamba, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuendelea kuimarisha barabara hizi za wilaya zinazosimamiwa chini ya TARURA. Ndiyo maana utaona tangu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani TARURA imeongezewa bajeti mara dufu. Bajeti kutoka shilingi bilioni 275 kwa mwaka, mpaka sasa ukijumlisha pamoja na fedha za nje, jumla ya shilingi bilioni 886 zinatengwa, kwa ajili ya barabara hizi za TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango na bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, TARURA imepanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 1.18. Kwa hiyo, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha barabara hizi za TARURA inaonekana kutokana na commitment ya kuongeza fedha. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itahakikisha inaendelea kufika katika maeneo mbalimbali ikiwemo Barabara hii ya Mkuyuni – Mahina – Nyakato, kwa ajili ya kuhakikisha barabara hii inajengwa kwa kiwango cha lami na inaweza kuwanufaisha wananchi. Kazi hiyo itaanza katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa urefu wa kilometa mbili. (Makofi)

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na juhudi za wananchi wa Ilemela kuendelea kufungua mtandao wa barabara za TARURA katika eneo na kufanya Ilemela ifunguke, lakini mpaka sasa tuna mtandao wa barabara kilometa 1,920. Serikali inahudumia barabara kilometa 875 na Manispaa ya Ilemela ni kati ya manispaa ambazo bajeti yake ya TARURA ni ndogo ukilinganisha na manispaa nyingine na majiji. Je, ni lini Serikali itaongeza fedha, kwa ajili ya TARURA na pia ku-cover mtandao wa barabara kama ambavyo wananchi wamefungua barabara za mji huo? Ahsante. (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula kwa swali lake ambalo linalenga kuimarisha Sekta ya Miundombinu ya barabara katika jimbo lake. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula kwamba, Serikali imesikia na itafanyia kazi kilio chako, lakini ninaomba nimhakikishie kwamba, bajeti ya TARURA inaendelea kuimarika kila mwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake hii bajeti itaendelea kufikia mtandao mkubwa zaidi wa barabara zetu hizi za wilaya. Kwa hiyo, kwa maombi yako haya mahsusi Serikali itayafanyia kazi, ili iweze kuongeza bajeti katika upande wa barabara za Ilemela. (Makofi)

Name

Iddi Kassim Iddi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Msalala

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 3

MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lililoko kwenye Barabara ya Mahina – Mkuyuni ni sawasawa na tatizo lililopo kwenye Barabara inayotoka Mwalugulu – Mwanase – Kabondo – Bulige. Barabara hii ndiyo kiungo kikubwa sana cha uchumi wa Jimbo la Msalala kwenye kata hizo nilizozitaja. Kwa kuwa, Serikali imetenga bajeti ndogo kwenye ukarabati wa barabara hiyo, ambayo kutokana na mvua zinazoendelea kwa sasa, ina hali mbovu sana. Sasa, ni nini mpango wa dharura wa Serikali kwenye kuongeza bajeti kuhakikisha ya kwamba, barabara hii inaenda kutengenezwa? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Iddi Kassim kwa swali lake zuri kabisa, ambalo linalenga kuimarisha miundombinu ya barabara katika jimbo lake. Ninaomba nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikiongeza bajeti ya TARURA kila mwaka. Tunatarajia katika mwaka wa fedha 2025/2026, bajeti ya TARURA itaongezeka mpaka kufikia shilingi trilioni 1.8. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake ni kwamba, fedha hizi zitaenda kufika katika mtandao mkubwa zaidi wa barabara zetu hizi za TARURA. Ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itafika katika barabara aliyoitaja, kwa ajili ya kuhakikisha inaijenga, inakuwa katika hali nzuri, ili iweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi iweze kuwawezesha kufikia huduma za kijamii. (Makofi)

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 4

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Serikali kuongeza pesa TARURA, kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika bajeti iliyopita Serikali iliahidi kununua vifaa, kwa ajili ya baadhi ya halmashauri ikiwemo Halmashauri ya Ukerewe, ambayo changamoto ni jiografia, vifaa kama greda na kadhalika. Ni hatua ipi sasa imefikiwa na Serikali kununua vifaa hivi, kwa ajili ya kurahisisha utengenezaji wa barabara kwenye halmashauri zetu? Ninashukuru.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Joseph Mkundi kwa swali lake hili zuri kabisa, ambalo linalenga kuboresha miundombinu ya barabara katika jimbo lake. Ninaomba nimhakikishie kwamba, Halmashauri ya Ukerewe tayari imeshafanya taratibu, kwa ajili ya kununua mashine mbalimbali ambazo zitatumika, kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge akae kwa mkao wa kupokea. Awataarifu wananchi wake kwamba, punde mashine hizi zitakapofika, basi wananchi wake watapata manufaa makubwa ya ukarabati na ujenzi wa barabara zaidi. (Makofi)

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 5

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ongezeko la bajeti ya TARURA, lakini fedha imekuwa haiendi kwa wakati. Changamoto zinatofautiana, Mheshimiwa Naibu Waziri, huoni kuna haja sasa ya kuangalia maeneo yenye changamoto kubwa na kuwe na programu maalum ya kuweza kumaliza changamoto hizo? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Aida Khenani kwa swali lake zuri, lenye maslahi mapana ya kuboresha miundombinu ya barabara, hasa hizi zinazosimamiwa na TARURA. Ninaomba niendelee kumweleza Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inatambua umuhimu mkubwa sana wa barabara hizi za wilaya ambazo zinasimamiwa na TARURA kiuchumi katika kuboresha mazingira ya wananchi wetu kufikia huduma za msingi za kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaweka mikakati ya kuhakikisha kwamba, inafika kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi, ikiwemo maeneo ambayo mawasiliano yamekatika na kuchukua hatua za dharura, kwa ajili ya kurudisha mawasiliano na kuhakikisha kwamba, wananchi hawakosi huduma muhimu hii ya barabara. Serikali itaendelea na mikakati hiyo pamoja na mingine kuhakikisha kwamba, inafika mara moja kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi, kwa ajili ya kuboresha miundombinu hii ya barabara hizi za TARURA, ili ziweze kuwanufaisha wananchi.

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 6

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Barabara ya Mbulu Mjini inayojengwa kwa kiwango cha lami, kipande, imesimama muda mrefu na kusababisha adha katika mji huo na mkandarasi ameondoka site. Je, ni lini mkandarasi huyo anatakiwa kurudi site na kukamilisha barabara hiyo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Yustina Rahhi kwa swali lake zuri linalolenga kuboresha miundombinu ya barabara katika Eneo la Mbulu Mjini. Ninaomba nitumie fursa hii, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwagiza Meneja wa TARURA, ngazi ya Mkoa na wa ngazi ya wilaya, kufanya ufuatiliaji kufahamu changamoto ya mkandarasi huyu ni nini, kutokukamilisha kazi yake na mkataba wake kwa wakati, waweze kuchukua hatua na kunipa taarifa.

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuiongezea fedha TARURA, ili kujenga Barabara za ndani, ikiwemo ya Mkuyuni – Mahina hadi Nyakato?

Supplementary Question 7

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Pofo – Mandaka – Kilema na Barabara ya Uchira – Kisomachi – Kolarie ni barabara zenye changamoto kubwa sana kule Vunjo. Nimekuwa ninazizungumzia kila wakati na nilifikiri kwamba, baada ya TARURA kupata ziada kutokana na ile Supplementary Budget uliyoipitisha hapa, basi fedha zingetiririka kwenye mkoa wetu wa Kilimanjaro, ili waweze kujenga upya au kukarabati barabara hizo. Je, ni lini sasa hizi fedha za ziada zitakwenda kwenye Mikoa, ili TARURA iweze kupata uwezo wa kujenga na ku-maintain barabara zile? (Makofi)

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei kwa swali lake hili zuri ambalo linalenga kuwasemea wananchi wake na hasa kwenye masuala ya barabara hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA katika jimbo lake. Ninaomba nimweleze Mheshimiwa Mbunge, ni kweli Bunge lilipitisha nyongeza ya bajeti na kupanga kutoa shilingi bilioni 50, kwa ajili ya dharura, kwenda kuhudumia barabara hizi za TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inafahamu changamoto alizozitaja za barabara katika jimbo lake na itachukua hatua stahiki, kwa ajili ya kuzifikia. Kwenda kujenga na kuzikarabati barabara hizo, ili ziweze kuwa katika hali nzuri, ziweze kuwanufaisha wananchi wako kiuchumi, lakini ziwawezeshe wananchi wako kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii. (Makofi)