Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 109 2025-04-22

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kujenga Daraja kuunganisha Kijiji cha Digoma na Digalama katika Mto Mjonga – Mvomero?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejenga daraja la muda la kamba za vyuma linalotumika na waenda kwa miguu pamoja na pikipiki, kwa ajili ya shughuli za usafiri na usafirishaji katika Kijiji cha Digoma na Digalama. Aidha, kazi ya usanifu wa daraja la kudumu lenye urefu wa meta 40 litakalojengwa kwa mawe imekamilika, kwa ajili ya ujenzi katika mpango wa fedha za dharura chini ya wabia Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ipo hatua za mwisho kwenye mchakato wa manunuzi, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Daraja la Mjonga katika Barabara ya Turiani – Digoma – Digalama linalounganisha Vijiji vya Kichangani, Muhonda, Digoma na Digalama. Serikali itaendelea kuuhudumia mtandao wa barabara Wilayani Mvomero kwa kuzijenga, kuzikarabati na matengenezo, kulingana na upatikanaji wa fedha.