Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kujenga Daraja kuunganisha Kijiji cha Digoma na Digalama katika Mto Mjonga – Mvomero?
Supplementary Question 1
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, majibu ya matumaini. Daraja hili ni muhimu sana kwa uchumi wa Watu wa Digoma, Digarama na Mvomero kwa ujumla. Kwa hiyo, ninaomba mchakato huo uharakishwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza; Barabara ya kutoka kwa Tembo Mchafu – Pemba – Gonja na Barabara ya kutoka kwa Tembo Mchafu – Kibogoji – Matindi – Pambambili – Diburumwa, wakandarasi wameondoka site na wamechimbachimba wameacha matope barabarani; ni adha kubwa sana kwa wananchi. Nikifuatilia ninaambiwa hawajalipwa. Je, lini Serikali itawalipa fedha zao walizoomba ili kazi hizi ziweze kuendelea? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Barabara ya kutoka Hembeti kwenda Kisimaguru yenye urefu wa kilometa nane, hii barabara tumeomba kupandishwa hadhi. Je, ni lini Serikali itaichukua hii barabara na kuipandisha hadhi? (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Van Zeeland Jonas kwa swali hili zuri kabisa, linalolenga kuwasemea wananchi wake katika jimbo lake kwa upande wa miundombinu ya barababara. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali inafanya ufuatiliaji wa kina kabisa kuhakikisha kwamba, wakandarasi wote wanaopewa mikataba, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara hizi za TARURA wanafanya hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumuagiza Meneja wa TARURA wa Mkoa, pamoja na Meneja wa TARURA wa Wilaya waweze kufanya ufuatiliaji kufahamu changamoto ya mkandarasi huyu, ambaye hayupo site, kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hii. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali imekuwa ikifanya kazi ya kuwalipa wakandarasi, kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, wanaendelea na kazi hizi za ujenzi wa barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha wiki mbili tu hizi, tayari jumla ya shilingi bilioni 335 zimeweza kutolewa kuwalipa wakandarasi, kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, wanaendelea na kazi. Hatua hizo zinaendelea kufanyika. Kwa hiyo, kama mkandarasi huyu ana madai yake, basi yaweze kuletwa katika ofisi zetu ili tuweze kufanya malipo na asiache kufanya kazi ya ujenzi muhimu kabisa wa barabara hizi kwa ajili ya wananchi wako.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, kuhusiana na kilometa nane za barabara aliyoitaja, ambayo anataka iweze kupandishwa hadhi. Ninaomba nitumie nafasi hii kuelekeza kwamba, utaratibu ule wa kupitisha maombi haya kwenye Bodi ya Barabara ya Mkoa yaweze kufanyika. Maombi yale yatapelekwa Wizara ya Ujenzi, kwa ajili ya hatua stahiki za kupandisha hadhi barabara hii kutoka hadhi ya Barabara ya Wilaya kwenda kwenye Barabara za Mikoa zinazosimamiwa na TANROADS.
							
 
											Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kujenga Daraja kuunganisha Kijiji cha Digoma na Digalama katika Mto Mjonga – Mvomero?
Supplementary Question 2
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwa kuwa, nyongeza ya bajeti ililenga kujenga madaraja kwenye maeneo korofi. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi katika Kijiji cha Mwamanongu, kama ilivyo kwenye mpango? (Makofi)
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Leah Komanya kwa swali lake zuri linalolenga kuboresha miundombinu ya barabara zinazozisimamiwa na TARURA katika jimbo lake. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Bunge lilipitisha nyongeza ya bajeti na kwenye nyongeza hiyo kulikuwa na shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuhudumia kwa dharura barabara hizi ambazo zipo chini ya TARURA. Ninaomba nimhakikishie, kwa kuwa daraja hili alilolitaja lipo kwenye mpango, Serikali itafika kwenye daraja hili ili kuchukua hatua za dharura kulijenga ili ziweze kuwanufahisha wananchi wake katika jimbo lake.
							
 
											Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kujenga Daraja kuunganisha Kijiji cha Digoma na Digalama katika Mto Mjonga – Mvomero?
Supplementary Question 3
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa swali la nyongeza, ninapenda kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Mchengerwa kwa kufanya ziara jimboni, ambapo alifika katika Hospitali yetu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiberege na akatoa maelekezo hospitali ile ianze mapema iwezekanavyo. Akiwa pale pale hospitali alipokea maombi ya Mheshimiwa Diwani ambaye alipiga goti kumwomba ujenzi wa Daraja la Mkasu ambalo lipo karibu na hospitali hiyo. Mheshimiwa Waziri, alitoa maelekezo kwamba ujenzi ule uanze mara moja na fedha zitafutwe. Mkandarasi amefika site, amemimina zege ile ya chini zaidi ya miezi miwili, mitatu sasa hivi mkandarasi yule haonekani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pale itapata hasara kwa sababu mvua zimeanza kwa kasi.  Je, ni lini Serikali itamfuatilia yule mkandarasi aweze kurudi site kumaliza Daraja lile la Mkasu Kata ya Kiberege? 
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Abubakari Asenga ambaye amekuwa akipaza sauti yake kwa ajili ya wananchi wake ili kuhakikisha kwamba miundombinu ya barabara hizi zinazosimamiwa na TARURA zinaimarishwa katika jimbo lake. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa alifika katika jimbo lake kwa ajili ya kufanya ziara na akatoa maelekezo ya ujenzi wa daraja hili la Mkasu. Hivyo, nichukue nafasi hii kumwagiza Meneja wa TARURA wa ngazi ya mkoa na wa ngazi ya wilaya kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kufahamu changamoto na kikwazo cha mkandarasi huyu kutekeleza wajibu wake kimkataba ni ipi na waweze kuchukua hatua na waweze kuwasiliana nami ili tuweze kuona tunafanyaje.
 
											Name
Anastazia James Wambura
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kujenga Daraja kuunganisha Kijiji cha Digoma na Digalama katika Mto Mjonga – Mvomero?
Supplementary Question 4
MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la Chekeleni Kata ya Kitere, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kuna daraja ambalo limekatika hivi karibuni na ni muhimu sana kwa kusafirisha mazao, kwa sababu pale Mtere ni eneo ambalo wanalima mazao mengi sana. Je, ni lini Serikali itajenga daraja hili katika eneo la Chekeleni?
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Anastazia Wambura kwa swali lake hili linalolenga kuwasemea wananchi katika Mkoa huu wa Mtwara katika wilaya hii kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na TARURA. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itafika katika eneo hili ambalo mawasiliano yamekatika kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inarudisha mawasiliano ili wananchi waweze kupata huduma nzuri ya barabara hizi na barabara hii na daraja hili liweze kuwanufaisha kiuchumi, lakini liweze kuwasasidia kufikia huduma za muhimu kabisa za kijamii.
 
											Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kujenga Daraja kuunganisha Kijiji cha Digoma na Digalama katika Mto Mjonga – Mvomero?
Supplementary Question 5
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.  Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itajenga Daraja kutoka Mwambiti, Itongolyangamba kwenda Buliashi Makao Makuu, daraja hili linaunganisha kata?
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itaondoa kero hiyo kwa wananchi wa Wilaya ya Meatu? 
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Minza Mjika kwa swali lake zuri kabisa hili. Niendelee kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara hizi za wilaya ambazo ni barabara muhimu kabisa kiuchumi. Pia ni barabara ambazo zinawawezesha wananchi kufikia huduma za muhimu za kijamii. Kwa hiyo daraja hili katika Wilaya hii ya Meatu litafikiwa na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba linajengwa na linaweza kuwanufahisha wananchi.