Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 110 2025-04-22

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:-

Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Tarime Vijijini lina vitongoji 500 ambapo vitongoji 225 tayari vina umeme, vitongoji 52 wakandarasi wapo wanaendelea na kazi, na vitongoji 82 zabuni ya kuwapata wakandarasi imetangazwa kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini awamu ya IIB. Zabuni hiyo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni. Aidha, vitongoji 141 vilivyosalia vitaendelea kupelekewa umeme kupitia miradi ijayo. Ahsante.