Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:- Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa katika awamu ya kwanza na ya pili ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia programu hii ya REA ilikuwa ikihusisha usafirishaji na usambazaji, lakini sasa hivi umeme umeshafika maeneo mengi katika vijiji kote nchini. Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kuongeza kasi katika kusambaza umeme kwenye vijiji kwa sababu tayari umeme umekwishafika katika maeneo mengi ya makao makuu ya vijiji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; wananchi wengi wameshalipia gharama zile za uunganishwaji umeme lakini mpaka sasa wengi bado hawajaunganishwa. Je, Serikali ipo tayari sasa kuongeza kasi ya uunganishaji umeme katika nyumba za watu ili watu hawa waweze kunufaika na huduma hii ya umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa maswali mazuri ya Mheshimiwa Mbunge ambayo yanaonesha ufuatiliaji wake wa kupeleka umeme na kusambaza umeme katika vitongoji. Serikali inao mpango wa kuongeza kasi ya kusambaza umeme kwenye vitongoji. Kama ambavyo wengi wanafahamu, katika kipindi cha miaka mitano Serikali imedhamiria kupeleka umeme katika vitongoji 20,000 kwa bajeti ya takribani trilioni 5.8; na kwa awamu ya kwanza tumeshatangaza sasa vitongoji 9,000 kwa ajili ya kuwatafuta wakandarasi, mradi ambao utagharimu takribani shilingi trilioni 1.5.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni azma ya Serikali kuendelea kuongeza kasi katika kusambaza umeme kwenye vitongoji ili kuwafikishia wananchi wengi zaidi na kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la pili la kuunganisha umeme, Serikali inayo mikakati ya kuendelea kuboresha na kufikisha huduma kwa haraka kwa wananchi. Tumejiwekea kwamba ndani ya siku 12 wateja waweze kuunganishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikiboresha bajeti ya ndani ya TANESCO na bajeti inayotoka Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ili kuirahisishia TANESCO kuendelea kupata fedha zaidi ili vifaa vinavyotumika katika kuunganisha umeme, kwa mfano nguzo, waya pamoja na mita, vipatikane kwa wepesi na wananchi waendelee kuunganishwa umeme kwa haraka. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba TANESCO inajizatiti kwa kweli na inaendelea kuboresha huduma kwa ajili ya kuwafikishia wananchi wengi zaidi na kuwaunganishia umeme kwa wakati. Ahsante.

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tanganyika

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:- Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Supplementary Question 2

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Azma ya Serikali ni kupeleka umeme vijijini kote. Kijiji cha Katobo ni Kijiji ambacho kipo kwenye Wilaya ya Tanganyika. Kijiji hiki hakijafikiwa na umeme. Je, ni lini Serikali itakipelekea kijiji hicho umeme ili uweze kuwanufahisha wananchi kwenye maeneo hayo?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vyote na kwa kweli ndiyo yaliyokuwa maelekezo kwa wakandarasi wote kuhakikisha kwamba wanapeleka umeme katika vijiji vyote. Kwa hiyo, kwa mahususi, kama Kijiji cha Katobo alichosema Mheshimiwa Mbunge bado hakijafikishiwa umeme basi nikitoka hapa nitafuatilia ili kuweza kujua changamoto ipo wapi na baada ya hapo tutafanyia kazi ili wananchi hawa na wenyewe waweze kupata umeme katika kijiji chao. Ahsante. (Makofi)

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:- Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Supplementary Question 3

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pale kwenye Jimbo la Igunga kuna vitongoji vilivyopo, kama vile kitongoji cha Ikulamawe, Mwalunju, Mwalugala, Ishemadilu na Mwalunili, viliingia kwenye mpango wa Serikali kupitia vitongoji kupatiwa umeme lakini mpaka sasa bado hatujapata feedback ya Serikali. Je, Serikali ina msimamo gani kuhusu vitongoji hivi ambavyo tayari vina idadi kubwa ya watu na shughuli nyingi za kiuchumi? Ahsante.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama vitongoji hivi anavyozungumzia Mheshimiwa Mbunge vipo katika Mradi wa Vitongoji 15 kwa kila Mbunge na kama vitongoji hivi vinakidhi vigezo ya kwamba viwe vimepitiwa na laini kubwa ili tuweze tu kufanya zoezi la ujazilizi, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa sasa wakandarasi wengi wamemaliza survey na sasa wapo katika zoezi la manunuzi na ukaguzi wa vifaa na baada ya hapo tutaendelea kuwaona kwa kasi katika majimbo yetu, kuanzia mwishoni mwa mwezi huu kwenda mwezi Mei. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama vitongoji hivyo vinakidhi vigezo hivyo basi hivi karibuni atawaona wakandarasi wanaendelea na kazi katika eneo lake.

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:- Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Supplementary Question 4

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Tarime ina baadhi ya maeneo ambayo yana hadhi ya vijiji au vitongoji na hayana umeme kabisa, kwa mfano, Kata ya Kitale maeneo ya Nkongole na Kata ya Nkende maeneo ya Mtalamloni. Je, ni lini Serikali sasa itapeleka umeme wa REA kwenye maeneo yote ya pembezoni katika halmashauri ya mji wa Tarime ambayo hayana umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo ambayo yapo mijini na katika maeneo ambayo yapo pembezoni mwa miji tunayo Miradi ya Peri-urban iliyopo na ambayo inakuja. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika miradi ambayo tunaiandaa tutahakikisha kwamba maeneo haya yanafikiwa. Kwa sasa tulishawaelekeza TANESCO Tarime watenge bajeti maalum kwa ajili ya kufikisha umeme kwenye ile mitaa ya pale ambayo haina umeme, at least kwa kuipunguza. Kwa hiyo nitafuatilia kuweza kujua wamefikia wapi katika kutafuta bajeti hiyo ili kuweza kupunguza adha kwa wananchi wa eneo la Tarime mjini. Ahsante.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:- Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Supplementary Question 5

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niwape pole Wizara kwa kuondokewa na Mtendaji Mkuu wa TANESCO ambaye anatokea Jimbo la Bunda Mjini, Kata ya Bunda Stoo, poleni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuuliza swali dogo la nyongeza. Tunajua kwamba umeme kwenye Jimbo la Bunda Mjini upo kwenye maeneo ya vijiji na zile kata saba za vijijini tayari kwenye vijiji umeshafika, lakini changamoto kubwa bado kwenye vitongoji. Wananchi wamekuwa wakilalamika kwamba wanahitaji umeme ili uwasaidie katika kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. Je, ni lini sasa mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji, kwenye Jimbo la Bunda Mjini utakamilika?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na kupeleka umeme kwenye maeneo ya Bunda Mjini ambayo yapo katika sura ya vitongoji. Tunayo miradi ambayo inakuja, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge; maeneo yale ambayo ni vitongoji nayo yapo katika mradi huu ambao tunaenda kuutekeleza. Aidha wa vitongoji 9,000 ama Miradi ya Peri-urban kwa maeneo kama haya ya Bunda Mjini. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tutaendelea kufanyia kazi ili na wananchi hawa waendelee kupata umeme.

Name

Halima James Mdee

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza:- Je, lini vitongoji vyote vya Jimbo la Tarime Vijijini vitapata umeme wa REA?

Supplementary Question 6

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikijenga hospitali za wilaya na shule za sekondari. Hapa ninazungumzia mikoa na halmashauri zote; lakini hakuna mikakati ya kuhakikisha kwamba maeneo husika yanapata umeme na matokeo yake ni kwamba majengo yapo lakini huduma za msingi hazifanyiki kwa sababu umeme hakuna. Sasa nilitaka jibu la kiujumla la mikakati ya Wizara kuhakikisha maeneo yote ya huduma za kijamii iwe ni shule, ziwe ni zahanati za wilaya, ziwe hospitali za mikoa. Je, kuna mkakati gani wa jumla wa kuhakikisha kwamba maeneo husika yanapata umeme?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge. Tayari Serikali imekuwa ina mikakati. Kupitia mradi wa fedha za Covid 19 tulishaanza mkakati, kupitia mradi wa zile fedha za Covid tulishaa..., samahani simaanishi ninyi. (Kicheko).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Mradi huu wa Fedha za Covid 19 Serikali iliweka mkakati wa kupeleka umeme kwenye taasisi; na kwa kweli tumekuwa tukifanya hivyo na tulishafikia zaidi ya taasisi 3,000 vituo vya afya pamoja na pampu za maji. vilevile tumekuwa na mradi mahsusi wa kupeleka umeme katika maeneo ya kuchagiza shughuli za kiuchumi kama migodi midogo pamoja na maeneo ambayo yanasaidia wananchi katika kuimarisha shughuli zao za kiuchumi. Kwa hiyo mkakati wa mwanzo ulishaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa miradi ambayo inaendelea mkakati mahsusi pia ni kuhakikisha kwamba tunavyopeleka umeme kwenye vijiji na vitongoji basi tunaanza kupeleka umeme kwenye taasisi husika zilizopo katika vijiji pamoja na vitongoji ili kurahisisha huduma za kijamii kwa wananchi, ikiwemo vituo vya afya, kielimu katika shule, pampu za maji pamoja na migodi midogo na maeneo yote ambayo yanaongeza uchumi katika jamii husika. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mikakati ipo tulishaianza na tunaendelea hivyo hivyo kwa miradi ambayo inafuatia.