Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 111 2025-04-22

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza:-

Je, lini suala la hedhi salama litapewa kipaumbele kwa kugawa taulo za kike bure shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu ya vyoo?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ilishaanza kutekeleza mpango wa hedhi salama katika shule za msingi na Sekondari kwa kutoa elimu juu ya masuala ya hedhi kwa lengo la kuvunja ukimya; uwekaji wa miundombinu ya kudhibiti bidhaa za hedhi, kuhakikisha watoto wa kike wanapata bidhaa bora na salama wakati wa hedhi pamoja na utoaji wa msaada wa kijamii. Baadhi wamekuwa wakipata maumivu makali wakati wa hedhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia inatekeleza Mwongozo wa Taifa wa Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Shuleni ambao umeweka maelekezo ya kila shule kutenga chumba kwa ajili ya kubadilishia sambamba na Mwongozo wa Usanifu wa Miundombinu ya Hedhi ambayo ni chumba cha kubadilishia ambacho kimeunganishwa na kiteketezi. Aidha, Mwongozo wa Uanzishaji na Usajili wa Shule 2020 umeweka chumba cha kujisitiri cha wasichana wakati wa hedhi kuwa miongoni mwa kigezo cha usajili wa shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.