Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Amina Ali Mzee
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza:- Je, lini suala la hedhi salama litapewa kipaumbele kwa kugawa taulo za kike bure shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu ya vyoo?
Supplementary Question 1
MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.  Swali la kwanza; je, Serikali haioni haja ya kuhakikisha wanajenga miundombinu ya vyoo ndani ya shule vya wanawake?
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni haja ya kutengeneza taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi kila shule? 
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
								NAIBU WAZIRI WIZARA YA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. Nianze kwa kumpongeza.  Kuna mwongozo mpya wa mwaka 2020 wa usajili wa shule umezingatia kwamba kunakuwa na chumba cha kujisitiri watoto wa kike na pia kunakuwa na kiteketezi. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, suala la kutengeneza hivyo vifaa kila shule, ni suala linalohitaji umakini, kunahitaji utengenezaji, lakini kuhakikisha kwamba vifaa hivyo ni salama. Kwa hiyo kulingana na uwezo, nafikiri ni kuhamasisha watu wengi wafanye; lakini tunahitaji control nzuri ili kuhakikisha kwamba zinavyofikia watoto basi zinakuwa salama na kwamba haziwezi kuwaletea madhara.
							
 
											Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza:- Je, lini suala la hedhi salama litapewa kipaumbele kwa kugawa taulo za kike bure shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu ya vyoo?
Supplementary Question 2
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Je, Serikali haioni kwamba ipo haja kwa kila shule kuwa na vyoo vyenye maji safi na salama ili kuweza kuwahudumia watoto hawa wanapokuwa kwenye hedhi?
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli ndio kinachofanywa na Serikali. Ndiyo maana hata ulivyoona fedha zile za Covid-19 zilivyokuja moja wapo ya maeneo yaliyoelekezewa fedha ni kwenye eneo la maji kuhakikisha kwenye maeneo ya shule moja spacing inakuwepo, lakini pia miundombinu ya maji kwenye shule zote inakuwepo.
 
											Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza:- Je, lini suala la hedhi salama litapewa kipaumbele kwa kugawa taulo za kike bure shule za msingi na sekondari na kuboresha miundombinu ya vyoo?
Supplementary Question 3
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mwongozo upo, lakini hautekelezwi na watoto wa kike hawapaswi kubadilisha nguo kwenye vyoo bali kwenye vyumba maalum vilivyoandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo. Ni ipi kauli ya Serikali ili kudhibiti shule zote zinazoanzishwa na zinazoendelea ziweze kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya watoto kujisitiri? Ninakushukuru. (Makofi)
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwongozo upo na ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mwongozo huo unatekelezwa na ndiyo maana kwenye ujenzi mpya sasa wa shule zetu ni mojawapo ya vigezo vya kusajili shule. Pia, sasa tuna zile shule zetu za zamani ambazo zina miundombinu ya zamani. Sasa inatekelezwa hatua kwa hatua kikubwa ambacho tunachokisema ni kuendelea kuhamasishana na kupitia kwa wenzetu wa TAMISEMI wameshatoa maelekezo maalum kwa Wakurugenzi ili kuhakikisha wakati wote wanatenga bajeti kwa ajili ya kuboresha maeneo kama hayo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved