Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 112 2025-04-22

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaagiza mazao ya mbaazi na ufuta kusafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mazao ya mbaazi na ufuta ni kati ya mazao yanayozalishwa na Mikoa ya Kusini mwa Tanzania na kuuzwa katika masoko ya Kimataifa. Tofauti na zao la korosho, usafirishwaji wa mazao hayo hufanyika, baada ya kusafishwa kwenye viwanda ambavyo vingi viko Dar es Salaam. Hivyo, usafirishaji hufanyika kupitia Bandari ya Dar es Salaam ambayo iko karibu na viwanda hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwezesha mazao ya mbaazi na ufuta kusafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara yakiwa na viwango vya masoko ya nje, Serikali kupitia Mamlaka ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imetoa Tangazo (Expression of Interest) la kukaribisha kampuni zilizo tayari kujenga miundombinu ya kusafisha mbaazi na ufuta karibu na maeneo ya uzalishaji Mkoani Mtwara na Lindi. Tayari kampuni tano zimejitokeza. Baada ya mchakato kukamilika zitaunganishwa na waendesha maghala ili kuwezesha kampuni hizo kukusanya na kuhifadhi mbaazi na ufuta kabla ya kuuza kupitia minada ya kidigiti.