Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hassan Seleman Mtenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Primary Question

MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:- Je, lini Serikali itaagiza mazao ya mbaazi na ufuta kusafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara?

Supplementary Question 1

MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali ya nyongeza mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali tayari imeshaleta mbolea kwa ajili ya zao la korosho na kwa sasa mvua zimeshaanza kunyesha Mkoa wa Mtwara maeneo mengi ya vijijini barabara huwa hazipitiki kwa wakati. Je, ni lini Serikali itaanza sasa kugawa mbolea hizo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, msimu wa mwaka jana kulikuwa na matatizo ambayo yalijitokeza kwenye vyama vya msingi, malipo kwa wakulima wa korosho yalikuwa yanasuasua sana. Je, Serikali imejipangaje kwa mwaka huu wa msimu malipo yaende sawa bila malalamiko kwa wananchi? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mheshimiwa Mtenga, kwa kufuatilia wakulima wake hususan wa zao la korosho. Jambo moja ambalo nimhakikishie tu kwamba sisi Serikali kupitia Wizara ya Kilimo tumetangaza mbolea inapofika ianze kusambazwa kwa wakulima. Nitumie forum hii kuwaambia wale mawakala wote wa usambazaji waanze kupeleka katika maeneo ambayo yamekusudiwa kuwafikia hususan katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu malipo ya korosho, Serikali tunaendelea kuboresha utaratibu ili kuhakikisha wanalipa kwa wakati na maelekezo ambayo aliyatoa Mheshimiwa Waziri katika mwaka uliopita kwamba mkulima alipwe ndani ya siku saba na utaratibu huo umeendelea kutekelezeka. Kwa hiyo, tutaendelea kufuatilia ili kuhakikisha mkulima hacheleweshewi malipo yake. (Makofi)