Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 113 2025-04-22

Name

Angelina Adam Malembeka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhifadhi mbegu na mimea ya asili kwa ajili ya vizazi vijavyo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa Serikali ni kuendelea kuhifadhi mbegu na mimea ya asili kwa ajili ya matumizi endelevu ya mbegu hizo. Hadi sasa, jumla ya sampuli 38,000 za mbegu na mimea ya asili zimekusanywa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuziendeleza. Kati ya hizo sampuli 10,000 zimehifadhiwa na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) kupitia kitengo cha Hifadhi ya Nasaba za Mimea na sampuli 28,000 zimehifadhiwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kukusanya mbegu hizo, Serikali imeanza taratibu za kujenga Benki ya Taifa ya Nasaba za Mimea (National Gene Bank) katika kituo cha TARI Selian (Arusha) ambapo kwa sasa michoro na makadirio ya ujenzi (BOQ) imekamilika kwa ajili ya kuendelea na hatua za kutangaza zabuni ya ujenzi. Ahsante sana.