Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 114 2025-04-22

Name

Kilumbe Shabani Ng'enda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:-

Je, nini mpango wa Serikali kujenga nyumba za Askari Polisi na Magereza eneo la Bangwe Kigoma Mjini?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la kambi ya Polisi Bangwe lina ukubwa wa meta za mraba 25,489.8 likiwa na nyumba za makazi ya Askari Polisi 42 wanazoishi familia 88. Katika eneo hilo Serikali ina mpango wa kujenga nyumba mpya nne za ghorofa zitakazoishi familia 48, kwani nyumba zilizopo sasa ni chakavu na haziwezi kukarabatika. Eneo la kambi ya Gereza Bangwe lina ukubwa wa ekari 52 likiwa na uwezo wa kukidhi idadi ya nyumba 61 za (two in one) za kutosheleza kwa makazi ya kuishi familia 123 za askari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Gereza Bangwe lina idadi ya nyumba 44 za kuishi familia 89 kukiwa na uhitaji wa nyumba 17 za kuishi familia 34. Aidha, kwa sasa Jeshi la Magereza, linaendelea na ujenzi wa nyumba mbili. Serikali kupitia Jeshi Polisi na Magereza itaendelea kutenga fedha kwenye Bajeti ya Serikali kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa nyumba pamoja na kuboresha makazi ya askari nchini ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Kigoma. Ahsante.