Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Kilumbe Shabani Ng'enda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigoma Mjini
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali kujenga nyumba za Askari Polisi na Magereza eneo la Bangwe Kigoma Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. KILUMBE S. NG'ENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Hata hivyo kama unavyofahamu mikoa yetu hii ya pembezoni imekuwa na matatizo ya watumishi wengi wa umma kutokupenda kufanya kazi huko. Swali la kwanza; je, Serikali haioni kwamba kuharakisha ujenzi huo ni kuhamasisha askari wetu kupenda kufanya kazi kwenye mikoa hii ya pembezoni? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, kwenye bajeti tunayoizungumzia ya mwaka huu wa 2025/2026 fedha hizo za kuanza ujenzi wa nyumba hizo za askari Magereza na Polisi eneo la Bangwe zimetengwa kwenye bajeti ili wawe na matumaini ya jambo hilo kukamilika? (Makofi)
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake makini sana kwa nyumba za askari wa Polisi pamoja na Magereza. Kuhusu maswali hayo mawili ya nyongeza. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la kwanza, ni kweli nia ya Serikali ni kuhakikisha kwamba askari wake wanakaa kwenye makazi bora ili waendelee kulinda usalama wa rai na mali zao. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali hii makini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan itahakikisha kwamba inaharakisha ujenzi wa nyumba za askari katika Mikoa ya pembezoni ikiwemo Mkoa wa Kigoma ili kuwavutia siyo kuvutia tu askari, lakini pia kutenda kazi ya kulinda raia na mali zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu jibu la swali la pili, kuhusu ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali itamalizia nyumba mbili ambazo zinajengwa kwa upande Jeshi la Magereza, lakini kwa Jeshi la Polisi ipo kwenye mpango na itatengewa bajeti kwa mwaka wa fedha  2026/2027. (Makofi)
							
 
											Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali kujenga nyumba za Askari Polisi na Magereza eneo la Bangwe Kigoma Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya askari wake wengi wanaishi uraiani kwa sababu nyumba za askari hazitoshi kiasi kwamba askari hao wanashindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mbarali hakuna nyumba, Kyela hakuna nyumba, Mbeya Jiji nyumba ni chache lakini pia Chunya hakuna na Mbeya DC hivyo hivyo. Sasa je, ni lini Serikali itajenga nyumba hizo kwa Askari wetu wa Mkoa wa Mbeya? (Makofi)
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Suma, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, kama ifuatavyo:- 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna upungufu wa nyumba za askari katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Mbeya, lakini Serikali imekuwa ikitenga fedha na kujenga nyumba awamu kwa awamu. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia Jeshi la Polisi itafanya tathmini katika Mkoa wa Mbeya na kuona kwamba yale maeneo ambayo yana upungufu mkubwa basi inatenga fedha na kuanza ujenzi wa nyumba za askari ili wakafanye kazi ya kulinda rai na mali zao.  Ahsante sana. (Makofi)
							
 
											Name
Khadija Hassan Aboud
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza:- Je, nini mpango wa Serikali kujenga nyumba za Askari Polisi na Magereza eneo la Bangwe Kigoma Mjini?
Supplementary Question 3
MHE. KHADIJA HASSAN ABOUD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Polisi Ziwani ni eneo ambalo wanaishi Maafisa wa Polisi na Polisi na kuna mali nyingi za kipolisi. Je, ni lini Serikali itajenga ukuta ili kunusuru maisha ya wanaoishi pamoja na vifaa vilivyomo? Kwa sababu sasa hivi uzio kwa nyuma umeanguka lakini mbele askari wanalinda ambapo mwananchi anaweza kupita kwa nyuma bila askari kumwona. Je, Serikali ni lini itajenga uzio katika eneo hilo? (Makofi)
 
											Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Khadija Aboud, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, niliagize Jeshi la Polisi, Kamishna upande wa Zanzibar kufanya tathmini ya eneo hilo la Ziwani ili kuhakikisha kwamba tunafanye tathmini tupate gharama ya ujenzi wa uzio huo na ili tuweze kutafuta fedha za kuzitenga kwa ajili ya ujenzi wa uzio ili askari wetu na mali zao waendelee kuwa salama.  Ahsante sana. (Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved