Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 115 2025-04-22

Name

Sylivia Francis Sigula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza:-

Je, lini zoezi la ulinzi kwa wavuvi wa Ziwa Tanganyika litaanza?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama imekuwa ikifanya doria kwenye maeneo mbalimbali ya Uvuvi ikiwemo Ziwa Tanganyika ili kudhibiti vitendo vya kihalifu na upotevu wa mali za wavuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo imeunda kikosi maalum kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya kihalifu ikiwemo vya kulinda usalama wa wavuvi wakati wakiwa katika maeneo yao ya uvuvi Ziwani na Baharini. Aidha, kikosi hicho kitafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia mwezi Aprili, 2025 hadi Mwezi Machi, 2026 katika maeneo yote ya Maziwa ikiwemo Ziwa Tanganyika pamoja na Bahari ya Hindi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuimarisha shughuli za ulinzi na usimamizi wa shughuli za uvuvi, Wizara imeanza kutumia teknolojia ya kisasa ikiwemo matumizi ya ndege nyuki kwa ajili ya kufuatilia vitendo vya uvuvi haramu na uhalifu katika maeneo yenye shughuli za uvuvi. Aidha, katika bajeti ya mwaka 2025/2026 Wizara imetenga jumla ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa ndege nyuki mbili ili kuimarisha shughuli za usimamizi ikiwemo ukanda wa Ziwa Tanganyika.