Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza:- Je, lini zoezi la ulinzi kwa wavuvi wa Ziwa Tanganyika litaanza?

Supplementary Question 1

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Serikali, upi mpango wa sasa uliopo kwa ajili ya kuiandaa jamii ya wavuvi inayoishi kandokando ya Ziwa Tanganyika ili kushirikiana na kikosi kazi hicho cha ulinzi kwa ajili ya kulinda mali zao na kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Kavejuru na nimthibitishie tu kwamba kabla ya mpango huu kuanza Wizara ya Mifugo na Uvuvi itatuma timu ya wataalam kwenda katika maeneo hayo ili kushirikiana na wananchi kuwaelimisha juu ya kikosi ambavyo kitakavyokuwa kinafanya kazi na kujenga ule ushirikiano kati ya wavuvi na wataalam ama kwa maana ya vikosi vya ulinzi na usalama. Kwa hiyo, hiyo ni sehemu ambayo Wizara imepanga kutekeleza na sasa hivi nilikuwa ninaongea na Katibu Mkuu amenihakikishia hilo kwamba timu ipo njiani kuelekea maeneo hayo kwa ajili ya kutoa elimu hiyo.