Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Water and Irrigation Wizara ya Maji 116 2025-04-22

Name

Shanif Mansoor Jamal

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwimba

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI K.n.y. MHE. SHANIF M. JAMAL aliuliza:-

Je, lini fedha za kuboresha mtandao wa maji kutoka Mhalo – Ngudu katika Jimbo la Kwimba zitalipwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafanya maboresho ya bomba la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Kijiji cha Mhalo kwenda Ngudu lenye umbali wa kilometa 25.4 kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Fedha za ujenzi wa mradi huo zinatarajiwa kupelekwa mwezi Mei, 2025 ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miezi 12. Uboreshaji wa mtandao wa maji kutoka Mhalo - Ngudu utakapokamilika utanufaisha wananchi wapatao 53,000 wa Mji wa Ngudu pamoja na Vijiji 16 vya Wilaya ya Kwimba vilivyopo kandokando ya bomba hilo.