Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NG’WASI D. KAMANI K.n.y. MHE. SHANIF M. JAMAL aliuliza:- Je, lini fedha za kuboresha mtandao wa maji kutoka Mhalo – Ngudu katika Jimbo la Kwimba zitalipwa?

Supplementary Question 1

MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu ya Serikali ambayo yanaendelea kusisitiza juhudi za Mheshimiwa Rais za kuhakikisha anaendelea kumtua mwanamama ndoo kichwani; nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; ni nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha unapunguza mgawanyo wa maji katika Vijiji vya Kadashi na Ngudu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inalipa wakandarasi wote waliopo katika miradi ya maji kwa wakati ili miradi yote inayotekelezwa ikamilike kwa wakati?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Ng’wasi Kamani, aliyeuliza kwa niaba ya Mheshimiwa Shanif Jamal Mansoor, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhamira ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kumtua mama ndoo kichwani, lakini kwa upande wa Mwanza katika kuhakikisha kwamba tunapunguza mgao, ndani ya Mkoa wa Mwanza ilitengewa kiasi cha shilingi bilioni 21 kutekeleza miradi 55.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kuna miradi ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Ukiliguru, Usagara, Mwamitinje pamoja na miradi ambayo inatekelezwa upande wa Hungumalwa ambapo katika miradi hiyo, takribani miradi 10 ipo katika Wilaya ya Kwimba. Ukiangalia katika Wilaya ya Kwimba zaidi ya shilingi bilioni 2.1 iliyokuwa imewekwa pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na huu mradi ambao Mheshimiwa Mbunge ameulizia, zaidi ya shilingi bilioni 6.2 Mheshimiwa Rais aliridhia kuzipeleka kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunakamilisha mradi huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni dhamira ya Serikali vilevile kuhakikisha kwamba miradi hii ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, wakandarasi lazima walipwe na warudi site ili kuhakikisha kwamba miradi hii inakamilika ili lengo la utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kufikia 85% kwa upande wa vijijini na 95% kwa upande wa mjini likamilike iliwemo na vijiji ambayo Mheshimiwa Mbunge ameviongelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha na ahsante sana.