Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Works and Transport Wizara ya Uchukuzi 117 2025-04-22

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:-

Je, nini haki za Abiria wa vyombo vya moto nchini na kwa kiwango gani wanatambua haki zao?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, abiria anayesafiri kwenye basi la njia ndefu (mikoani na nchi jirani), basi la mjini (daladala), teksi, pikipiki za magurudumu mawili au matatu, treni, ndege, pamoja na meli ana haki ya usalama wa chombo na mazingira salama, haki ya kuchagua chombo cha usafiri, haki ya kulipwa fidia pale anapostahili kama akipata majanga, haki ya kusikilizwa na kuelimishwa, haki ya kupewa tiketi na kufikishwa mwisho wa safari yake.