Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 9 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 118 2025-04-22

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa ziada wa kulinda haki za watoto, kwani kuna ongezeko kubwa la uvunjifu wa haki za watoto nchini?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Serikali itaendelea kuweka mikakati ya ziada ya kulinda haki za watoto nchini. Aidha, mikakati hiyo ni pamoja na:-

(i) Kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa 2024 - 2029 unaolenga kutokomeza ukatili kwa 50% ifikapo mwaka 2029;

(ii) Kuelimisha jamii kuhusu Sheria za Ulinzi wa Mtoto, mathalani mtu anayekutwa na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 na Wazazi wasiolea na kutunza watoto adhabu ni faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo miezi sita au vyote kwa pamoja

(iii) Kuendelea kuibua Kampeni za kuelimisha Jamii kuhusu Haki za Watoto, mfano Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (2023 - 2025), pamoja na;

(iv) Kuimarisha mkakati wa ulinzi na usalama wa mtoto kwenye Jamii pamoja na Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto kwenye Shule za Msingi na Sekondari.