Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa ziada wa kulinda haki za watoto, kwani kuna ongezeko kubwa la uvunjifu wa haki za watoto nchini?

Supplementary Question 1

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninawashukuru Serikali kwa namna ambavyo wanafanyia kazi mambo ya ustawi wa jamii na kupokea mashauri mengi ya Waheshimiwa Wabunge ambayo tunayatoa. Hata hivyo, nina maswali mawili. Swali la kwanza; kuna baadhi ya wazazi na walezi bado wana tabia ya kuwaozesha watoto ambao bado hawajapea kifikra na hivyo kusababisha ndoa zao kutodumu. Je, Serikali ina mpango au mkakati gani wa kuwafikia watoto hawa ili waweze kupata haki yao ya kimsingi ya kielimu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa mustakabali mzuri wa kudhibiti mporomoko wa maadili katika Taifa letu; je, Serikali lini itaandaa Sera ya Taifa ya watoto na vijana ili kuweza kuweka mfumo ulio imara kwa wazazi, walezi na Serikali kudhibiti mporomoko wa maadili katika Taifa letu?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Najma Giga, kwa vile yeye ni Mbunge kupitia Jumuiya ya Wazazi basi ana haki ya kulinda na kukuza malezi ya watoto wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la mwanzo linasema kwamba ni wajibu wa kisheria mzazi au mlezi kulea mtoto wake hadi anapofikia umri wa miaka 18. Sheria hii imetungwa na Serikali sura Na. 13, Sheria ya Elimu ya mwaka 2022 inamlinda mtoto kuhakikisha anapata elimu. Vilevile, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kujengwe shule za boarding katika mikoa yote ya Tanzania. Hii ni kwa sababu ya kuwalinda watoto wa kike waondokane na ukatili wa kijinsia ambao wanaupata katika jamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, Serikali inaendelea kutekeleza Sera ya Mtoto ya mwaka 2008 na Sheria ya Vijana ya mwaka 2007. Hii ni kutokana na utandawazi ambao unaendelea, Serikali inaendelea kubadilisha marekebisho ya sheria kadri tunavyokwenda kutokana na utandawazi na tabianchi ambayo tunaendelea nayo ili kuondoa mmomonyoko wa maadili katika nchi yetu.