Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 484 2025-06-03

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka huduma ya x-ray machine kwenye Vituo vya Afya Nkende na Kibumaye – Tarime?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI A MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa huduma za kiuchunguzi za mionzi katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi nchini. Katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2024/2025 jumla ya mashine za kidijiti za x–ray 318 zimenunuliwa na kufungwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini. Aidha, Halmashauri ya Mji Tarime imepokea mashine mbili za x–ray na kuzifunga katika Hospitali ya Nyamwaga na Kituo cha Afya cha Sirare.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya kununua mashine za x–ray na kuzipeleka kwenye vituo vya afya vitakavyokuwa vimekamilisha ujenzi wa majengo ya huduma za mionzi kote nchini vikiwemo Vituo vya Afya vya Nkende na Kibumaye katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.