Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka huduma ya x-ray machine kwenye Vituo vya Afya Nkende na Kibumaye – Tarime?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni takribani miezi miwili sasa x-ray machine iliyopo katika Hospitali ya Mji wa Tarime haifanyi kazi kabisa na wamekuwa wakiifanyia ukarabati mara kwa mara inaonekana imechoka na kwa sababu Halmashauri ya Mji ya Tarime inatoa huduma hii siyo tu kwa wakazi wa Mji wa Tarime, bali wa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Rorya.  
Je, Serikali haioni kwamba kuna haja sasa ya kupeleka x-ray machine walau mbili ambazo zinafanya kazi na mpya ziweze kuwahudumia wananchi hawa, ili moja ikiharibika nyingine iweze kufanya kazi?
 
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, pamoja na majengo mazuri ambayo tuna-appreciate mmetujengea Hospitali wa Tarime likiwepo lile la emergency, lakini bado kumekuwa na changamoto ya vifaa vingine vya kuweza kusaidia kutoa huduma bora. Kwa mfano mashine iliyopo ambayo ni washing machine ya kuweza kufua mashuka ya wagonjwa imeharibika na ni ya muda mrefu. 
Je, Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka sasa wa kupeleka washing machine mpya ya kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi wale wa Mji wa Tarime na wengine wanaokuja kupata huduma pale?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI A MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika dhamira muhimu sana ya Serikali ni kuhakikisha vituo vya huduma za afya, hospitali za halmashauri zinapima magonjwa kwa kutumia vifaa vya kisasa. Moja ya vifaa hivyo ni mashine za x-ray, na ndiyo maana Serikali imenunua zaidi ya x-ray 318 za kidijiti katika miaka hii miwili na zimepelekwa kwenye vituo vya afya. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuiana na mashine ya x-ray katika Hospitali ya Mji wa Tarime kuharibika, ni suala la dharura. Natumia nafasi hii kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Mganga Mkuu wa Halmashauri na Mganga Mkuu wa Mkoa kufanya tathmini ya haraka kuona namna gani x-ray mashine hiyo inatengenezwa na kuanza kutoa huduma mapema iwezekanavyo na ikiwa mashine hiyo haitengenezeki walete taarifa mapema ili tuweze kuwasiliana na Bohari ya Dawa (MSD) na kupata mashine nyingine ili kuhakikisha kwamba tunarejesha huduma za x-ray, katika hospitali hiyo ya halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, vifaa tiba vinanunuliwa na Serikali Kuu lakini pia kuna vifaa ambavyo vinanunuliwa na halmashauri yenyewe ikiwemo mashine za kufulia. Kwa hiyo, nitumie nafasi hii kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi pia kuona uwezekano wa kununua mashine ambayo ipo ndani ya uwezo wa mapato ya ndani ya halmashauri ili huduma hizo ziweze kurejea katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime. (Makofi)
							
 
											Name
Sylivia Francis Sigula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka huduma ya x-ray machine kwenye Vituo vya Afya Nkende na Kibumaye – Tarime?
Supplementary Question 2
MHE. SYLIVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Nkasi, Kata ya Kate, tunamshukuru Mheshimiwa Rais ametujengea kituo cha afya na vifaa vimeenda vya kisasa, lakini hakuna wataalam wa ku-operate vifaa hivyo na hospitali hiyo haifanyi kazi.
Je, ni lini mtapeleka wataalam ili Kituo cha Afya cha Kate kiweze kufanya kazi?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI A MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ajira zote ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ikiwemo ajira 34,720 za watumishi wa sekta ya afya ambazo zimetolewa katika kipindi hiki cha miaka minne. Moja ya wataalam ambao wamekuwa wakiajiriwa ni wataalam wa mifumo, vifaa tiba, x-ray, ultrasound na wengine kama maabara na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie tu Mheshimiwa Sigula kwamba Serikali inatambua baadhi ya maeneo bado kuna upungufu wa wataalam hao, lakini tumeshatoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya reallocation ya watumishi ndani ya mkoa na ndani ya halmashauri ili vile vituo ambavyo vina upungufu mkubwa zaidi vianze kutoa huduma za msingi wakati vibali vya ajira vikiendelea kutolewa. 
Mheshimiwa Mbunge kwa hiyo, nikuhakikishie tu kwamba tutafuatilia hilo na kuhakikisha wataalam hao wanapelekwa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hizo muhimu.
							
 
											Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka huduma ya x-ray machine kwenye Vituo vya Afya Nkende na Kibumaye – Tarime?
Supplementary Question 3
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Kituo cha Afya Kiponzelo kilichopo katika Jimbo la Kalenga, Kata ya Maboga, kinahudumia zaidi ya vijiji vitano na kuna changamoto ya x-ray ambayo ni mbovu kwa muda mrefu. 
Je, hamuoni sasa kuna haja ya kupeleka hizo x-ray mashine ambazo mmezitoa ziende katika kituo cha afya hicho ili kiwasaidie wananchi wa pale?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI A MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 ambao tunauhitimisha, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 63.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba zikiwemo digital x-rays na tayari tumeshaainisha vituo vya afya ambavyo vina ukosefu wa mashine hizo kikiwemo Kituo cha Afya cha Kiponzelo ambacho tulishapata taarifa Mheshimiwa ameuliza zaidi ya mara mbili. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshaingiza kwenye orodha hiyo na tunaamini wakati wowote manunuzi yakikamilika, tutapeleka mashine ya x-ray katika Kituo cha Afya cha Kiponzelo.
							
 
											Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka huduma ya x-ray machine kwenye Vituo vya Afya Nkende na Kibumaye – Tarime?
Supplementary Question 4
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na shughuli za kiuchumi kule Tarime, uchimbaji, pamoja na shughuli za bodaboda kuna ajali nyingi sana Tarime Vijijini na Wilaya ya Tarime kwa ujumla. Ni lini mpango wa Serikali kupeleka x-ray mashine katika Kituo cha Afya Bumela, Sungusungu, Kerende, Magoma pamoja na Mtana ili watu wangu waweze kupata huduma za x-ray machine?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la ajali na hususan ajali za pikipiki maarufu bodaboda ambazo mara nyingi sana majeruhi wanahitaji kupata huduma za x-ray kama Mheshimiwa Waitara alivyosema na ndio maana Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaatiba zikiwemo mashine za x-ray. Tayari katika Halmashauri ya Tarime Vijijini wamepata x-ray na tunaendelea na taratibu za manununzi kwa ajili ya kupeleka x-ray katika vituo ambavyo Mheshimiwa Mbunge amevitaja. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge vituo ulivyovitaja tutakwenda kwa awamu kuhakikisha kwamba tunapeleka mashine za x-ray. (Makofi)
 
											Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka huduma ya x-ray machine kwenye Vituo vya Afya Nkende na Kibumaye – Tarime?
Supplementary Question 5
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi. Halmashauri ya Rorya ina vituo vya afya vinne kwa maana ya Utegi, Nyamagaro, Kinesi pamoja na Rabour, lakini vituo vya afya vyote hivi vinne havina Jengo la Mionzi (x-ray) na wala hawana mashine za x-ray. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili na ununuzi wa kifaa hiki cha x-ray?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ujenzi wa majengo ya x-ray katika vituo vyetu vya afya yanafanyika kwa vyanzo mbalimbali vya mapato zikiwemo fedha za mapato ya ndani pia fedha kutoka Serikali Kuu. 
Kwa hiyo, ninaomba kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Chege kwamba Serikali inatambua lazima tuwe na majengo hayo ya x-ray na nitumie nafasi hii kumuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya kwanza kutenga fedha kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo ya x-ray angalau kwenye vituo viwili vya afya wakati Serikali Kuu ikitafuta fedha kwa ajili ya kwenda kujenga majengo hayo. Nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge lazima Serikali itakwenda kujenga majengo hayo na pia kupeleka mashine za x-ray ili vituo hivyo viwe na huduma zote muhimu.