Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 485 2025-06-03

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya Chifutuka kilipokea shilingi milioni 500 mwaka 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara, jengo la upasuaji, jengo la wazazi, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi. Ujenzi wa majengo hayo umekamilika na majengo yanatumika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya kukamilisha miundombinu inayopungua katika Kituo cha Afya cha Chifutuka.