Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza. 
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya cha Magubike ikiwemo ujenzi wa wodi ya wanaume pamoja na chumba cha watoto njiti?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, ni lini Serikali itapeleka wafanyakazi wa kutosha wa afya kwenye vituo vya afya Mkoani Morogoro? Ahsante.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Mbunge mama yangu Dkt. Christina Ishengoma ameuliza mara kadhaa kuhusiana na ujenzi wa wodi hizo, wodi ya wanaume pia chumba wodi ya watoto njiti katika Kituo cha Afya cha Magubike. Tayari tulishakubaliana Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuingiza Kituo cha Afya cha Magubike kwenye vituo vya kimkakati ambavyo fedha kupitia Mfuko wa Benki ya Dunia utakwenda kujenga miundombinu hiyo inayosalia. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tayari inaendelea na taratibu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa majengo hayo. (Makofi) 
							
 
											Name
Selemani Moshi Kakoso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tanganyika
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 2
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi. Kwanza niishukuru na kuipongeza Serikali kwa kujenga miundombinu ya vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika. (Makofi) 
Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika ina mtaalam mmoja tu wa mionzi ambaye anafaya kazi kwenye vituo vya afya na hospitali ya wilaya. Ni lini mtampeleka msaidizi wake ili aweze kufanya kazi vizuri kwa wananchi? (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Hospitali ya Halmashauri ya Tanganyika ina mtaalam mmoja wa x-ray na tunafahamu kwamba tunahitaji kuwa na wataalam angalau wawili au watatu ili kuwa na uhakika na huduma za afya pindi yule mtaalam mmoja anapopata dharura. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali imeendelea kuajiri wataalam hao, lakini kimsingi wataalam hao wapo wachache kwenye soko na mpango wa Serikali tumeendelea kufanya mafunzo ya muda mfupi kwa wataalam wa sekta ya afya waliopo kazini ili waende kuziba pengo la wataalam wa x-ray katika halmashauri zetu. Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Kakoso kwamba baada ya wataalam hao waliopo kwenye kozi za muda mfupi kuhitimu tutahakikihsa tunaleta wataalam katika Hospitali ya Tanganyika ili kuondoa pengo la watumishi katika sekta hiyo.
							
 
											Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 3
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, mwaka 2022/2023 Serikali ilikuwa na mpango wa kujenga vituo vya afya kwenye kata zote za mipakani. Moja ya kata hizo ilikuwa ni Kata ya Mpendo, Jangalo, Lahoda na Kinyamshindo kwenye Jimbo la Chemba. Ninataka kujua huo mkakati uliishia wapi? Ahsante.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi wa mwaka 2007 – 2017 ambao ulikuwa unaelekeza ujenzi wa kituo cha afya kwenye kila kata na ujenzi wa afya kwenye kila kijiji, lakini Serikali ilifanya tathmini na kuona uhalisia wa utekelezaji wa mpango huo na tija ya kuwa na mpango huo Serikali ikaja na mpango mwingine mbadala, kwamba badala ya kujenga kituo cha afya kwenye kila kata tutajenga vituo vya afya kwenye kata za kimkakati ambazo zitakidhi vigezo vya idadi ya watu angalau 15,000 na umbali kutoka kituo cha afya cha jirani zaidi angalau kilometa tano. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Monni kwamba vile vituo vya afya ambavyo vinakidhi vigezo vya kata za kimkakati Serikali itaendelea kuandaa mpango kwa ajili ya kwenda kujenga vituo hivyo vya afya, vile ambavyo havikidhi vigezo vitapata huduma katika maeneo ya karibu na vituo vingine ambavyo vitakuwa na vituo vya afya.
							
 
											Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 4
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha Vituo vya Afya vya Idiwili, Luanda na Isangu, Vwawa?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Luanda, Kisangu na hicho kingine ambacho Mheshimiwa Hasunga amekitaja ni miongoni mwa vituo vya afya ambavyo Serikali imeshapeleka fedha na kuanza ujenzi wa miundombinu awamu ya kwanza. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ujenzi wa vituo hivi vya afya unafanyika kwa awamu. Tulianza na awamu ya kwanza ya majengo ya OPD, maabara, kichomea taka na mengine ili huduma za msingi zianze lakini tutakwenda awamu ya pili kwa ajili ya kujenga majengo yanayopungua ikiwemo wodi na majengo mengine. 
Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Hasunga kwamba Serikali inaendelea kutekeleza mpango huo na tutafika kukamilisha majengo hayo katika Jimbo la Vwawa.
							
 
											Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 5
MHE.  DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi kuuliza swali la nyongeza. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuna Hospitali ya Wilaya pale Iselamagazi lakini kuna baadhi ya majengo hayajakamilika ikiwepo wodi za wanawake na wanaume. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kukamilisha majengo hayo?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumefanya ziara katika Hospitali ya Halmashauri ya Shinyanga. Yapo majengo ambayo yamekamilika, lakini yapo majengo ambayo bado hayajakamilika na kuna majengo ambayo yanahitajika. Serikali ilishatekeleza awamu ya kwanza ya ujenzi wa majengo yale kwa kupeleka zaidi ya shiingi bilioni mbili. Tunaendelea na mpango mwingine kwa ajili ya kukamilisha majengo ambayo hayajakamilika. 
Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Christina kwamba Serikali tayari imeweka mpango kwa ajili ya kwenda kukamilisha majengo hayo mengine ili hospitali ile iwe na majengo yote muhimu na itoe huduma ambazo zinatarajiwa kwa wananchi.
							
 
											Name
Deo Kasenyenda Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makambako
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 6
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona. Nimekuwa nikikumbusha sana Serikali juu ya kujenga kituo cha afya katika Kata ya Kivavi na Serikali imeniahidi kwamba tutapewa kituo kimoja katika Halmashauri ya Mji ya Makambako. 
Je, ni lini sasa tutapatiwa fedha hizo za kujenga kituo cha afya katika Kata ya Kivavi?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makambako mara kwa mara amefuatilia sana kuhusiana na uhitaji wa kujenga kituo cha afya katika Kata ya Kivavi na kwa bahati nzuri tayari Serikali imeshaweka kata hiyo kwenye mpango wa Benki ya Dunia kwa ajili ya kwenda kujenga kituo hicho cha afya. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Deo Sanga kwamba tunasubiri tu suala la utaratibu wa kifedha na mara taratibu zikikamilika tutaanza ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Kivavi. (Makofi)
							
 
											Name
Kasalali Emmanuel Mageni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sumve
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Chifutuka – Bahi?
Supplementary Question 7
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru, Kituo cha Afya cha Nyambiti katika Jimbo la Sumve ni kituo cha afya cha kimkakati kwa sababu kipo Makao Makuu ya Jimbo. Pia ni kituo cha afya ambacho hakina jengo la upasuaji na wananchi walifanya juhudi kubwa kulijenga na tukapata na mfadhili akatuletea mpaka vifaa, lakini vifaa hivyo vinaharibika kwa sababu ya kukosekana kwa jengo. 
Je, ni lini Serikali itatuunga mkono sisi wananchi wa Sumve katika kujenga jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Nyambiti?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge amefuatilia mara kadhaa kuhusiana na suala hili. Ni kweli kwamba Kituo cha Afya cha Nyambiti kina upungufu wa majengo na tulishamuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba kuleta taarifa ya fedha zinazohitajika kujenga jengo la upasuaji, ili huduma za upasuaji zianze katika Kituo cha Afya cha Nyambiti. 
	Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba nitumie nafasi hii kumkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba kuleta mapema iwezekanavyo makadirio ya mahitaji ya fedha kwa ajili ya kujenga jengo la upasuaji ili vifaa hivyo vianze kutumika na wananchi wa Kwimba wapate huduma ambazo zinastahili.