Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 486 2025-06-03

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza kujenga mifumo ya uvunaji maji ya mvua katika shule zote nchini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, sensa ya elimu msingi ya mwaka 2024 inaonesha kuwa shule 5,311 za sekondari zina vyanzo vya maji vya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 2,960, visima ni shule 1,217 na wanaovuna maji ya mvua ni shule 1,134. Aidha, shule 20,509 za msingi zina vyanzo vya maji vya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 10,965, visima shule 4,966 na shule zinazovuna maji ya mvua ni 4,578.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati ya Serikali ya kufikisha huduma za maji safi na salama katika shule za msingi na sekondari nchini ni pamoja na ujenzi wa shule mpya au miundombinu ya vyoo kujumuisha fedha za ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa itaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha shule zinakuwa na huduma ya maji safi na salama, kwa kuzingatia vyanzo vya maji vya eneo husika.