Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 487 2025-06-03

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -

Je, lini Serikali itakarabati mabweni ya wasichana ya kidato cha tano na sita katika Shule za Kilindi na Mlongwema?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitoa fedha za ujenzi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali katika Shule za Wasichana Kilindi na Mlongwema kwa ajili ya kuboresha mazingara ya ujifunzaji na ufundishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 Serikali imetoa shilingi milioni 312 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne, bweni moja, umaliziaji wa bweni moja na bwalo moja katika Shule ya Wasichana Kilindi. Aidha, bweni lililokamilishwa ni ambalo lilikuwa chakavu kutokana na kuanza kutumika kabla ya ukamilishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa shilingi milioni 578.5 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili, madarasa 11, matundu 17 ya vyoo na ukarabati wa mfumo wa maji wa bweni katika Shule ya Sekondari Mlongwema. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati au ujenzi wa miundombinu katika maeneo mbalimbali katika shule za kidato cha tano na sita ili kuboresha mazingira ya elimu nchini. (Makofi)