Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, lini Serikali itakarabati mabweni ya wasichana ya kidato cha tano na sita katika Shule za Kilindi na Mlongwema?
Supplementary Question 1
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati natembelea hizo shule hali ilikuwa ni mbaya na hairidhishi, hali siyo nzuri kwa ujumla. Mabweni yapo kwenye hali mbaya. Je, Serikali ina mkakati madhubuti na mahsusi kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa mabweni katika shule hizi mbili? (Makofi) 
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafahamu ujenzi unafanyika kutokana na upatikanaji wa fedha, je, kuna mpango gani wa kukarabati majengo haya ili kuwasaidia watoto wanaosoma pale angalau kuwa katika mazingira yanayovutia? Ahsante sana. 
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali imeweka mpango mkakati kwanza kwa kuainisha maeneo au shule ambazo zina miundombinu chakavu yakiwemo mabweni, mabwalo na madarasa na Serikali imekuwa ikitenga fedha katika kila bajeti kupitia programu mbalimbali ikiwemo SEQUIP kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mabweni na miundombinu mingine inajengwa. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Sekiboko kwamba kwa hali ya mabweni katika hizi Shule za Sekondari ya Kilindi na Mlongwema, Serikali itaweka kipaumbele kutafuta fedha mapema iwezekanavyo na kwenda kukarabati mabweni hayo ili wanafunzi waweze kuishi katika mabweni bora zaidi na kuweza kupata elimu katika mazingira mazuri zaidi. (Makofi)
							
 
											Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, lini Serikali itakarabati mabweni ya wasichana ya kidato cha tano na sita katika Shule za Kilindi na Mlongwema?
Supplementary Question 2
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo katika Shule ya Sekondari ya Kilindi kutokuwa na mabweni, kumekuwa na shida ya mabweni katika Shule ya Sekondari ya Ikuti Wilaya ya Rungwe, wananchi na halmashauri imejitahidi sana kujenga na kufikia ngazi ya lintel, ni lini Serikali mtaona sasa ni wajibu wenu kupeleka fedha ili kuweza kumalizia mabweni yale? (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kila mwaka wa fedha kwa ajili ya kukamilisha mabweni na miundombinu mingine ya shule, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe pia ni moja ya shule ambazo zimepelekewa fedha nyingi sana kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, mabwalo, madarasa na shule nyingine mpya. Kwa hiyo, Serikali imekuwa ikitimiza wajibu huo kwa dhati kabisa na ninakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kwanza niwapongeze wananchi wa Rungwe kwa kuchangia nguvu zao katika Shule ya Sekondari ya Ikuti kwa ajili ya kujenga mabweni, ni jambo zuri na Serikali tayari imechukua stock ya maboma hayo kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kupeleka fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunakamilisha mabweni haya. (Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved