Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 488 2025-06-03

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaoendelea katika Mji wa Mpwapwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatekeleza ujenzi wa barabara kwa tabaka la lami na uwekaji wa taa 41 katika Mji wa Mpwapwa kwa mikataba miwili yenye thamani ya shilingi bilioni 1.11 ambapo kilometa tatu zinajengwa. Mradi huo umefikia 70% na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuihudumia miundombinu ya barabara na madaraja ya Mji wa Mpwapwa kwa kuijenga, kuikarabati na kuifanyia matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha. (Makofi)