Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaoendelea katika Mji wa Mpwapwa?
Supplementary Question 1
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara kwa tabaka la lami katika Mji wa Mpwapwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano. Ahadi ilikuwa ni kujenga kilometa 10 za tabaka la lami, lakini sasa hivi ujenzi unaoendelea ni wa kilometa tatu tu. 
Ni nini tamko la Serikali kwa kilometa saba zilizobaki? (Makofi)
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tamko la Serikali ni kwamba tayari imeanza kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano na kujenga kilometa hizo 10 za barabara ya lami katika Mji wa Mpwapwa na ndiyo maana tumeanza na kilometa tatu, tutaendelea kwa awamu katika kila mwaka wa bajeti kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo. (Makofi)
 
											Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaoendelea katika Mji wa Mpwapwa?
Supplementary Question 2
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru nami kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. 
Barabara ya Kisawio - Mamandizi ambayo inaelekea Kituo cha Afya cha Uru Kusini kilichojengwa kwa gharama kubwa sana za Serikali, haipitiki na inapelekea wananchi wagonjwa kubebwa kwa machela. Ni lini Serikali itajenga barabara hii kwa kuwa nimeuliza mara kwa mara na kujibiwa inajengwa, ni lini Serikali itaijenga barabara hii? (Makofi) 
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya vipaumbele vya Serikali ni kuhakikisha maeneo yote ya huduma za kijamii yanakuwa na barabara bora zinazopitika na hususani maeneo ya huduma za afya lazima tuweke kipaumbele kuhakikisha kwamba barabara zinapitika, kwa sababu ni maeneo ambayo yanakuwa na magari ya wagonjwa na wagonjwa mahututi wanahitaji kuwahishwa kwenye vituo vingine vya rufaa. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa ni kweli ameuliza mara kadhaa na Serikali tumempa commitment, taratibu zinazoendelea ndani ya Serikali ni kufanya tathmini ya gharama ya fedha zinazohitajika kwa ajili ya barabara hiyo na kupeleka fedha mapema iwezekanavyo kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo. 
Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali hii ni sikivu inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, itakwenda kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo ili wananchi wa Kituo cha Afya cha Uru Kusini wapate huduma bora zaidi. 
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved