Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 489 2025-06-03

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kada nyingine wanapewa madaraja mserereko kama ilivyo kada ya ualimu?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298 jukumu la kuwapandisha vyeo watumishi ni la mwajiri husika. Jukumu hili hutekelezwa baada ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutoa mwongozo kuwataka waajiri kuandaa na kuwasilisha ikama na bajeti ya mwaka husika wa fedha na ofisi kuridhia utekekelezaji wa bajeti hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imewapandisha vyeo kwa mserereko watumishi wasio walimu 1,284. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetoa mwongozo unaohusu upandishaji vyeo na ubadilishaji kada ikiwemo na kwa watumishi waliocheleweshwa kupandishwa vyeo. Hivyo, nitoe wito kwa waajiri wote katika sekta ya umma kutekeleza kwa wakati mwongozo huo ili kuepusha malalamiko kwa watumishi wa umma wenye changamoto za kupandishwa vyeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.