Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kada nyingine wanapewa madaraja mserereko kama ilivyo kada ya ualimu?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa kazi kubwa waliyofanya kupandisha madaraja ya watumishi Tanzania, lakini pamoja na pongezi hizo ninayo maswali madogo mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, je, Serikali ina mkakati gani kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo hii wanayoituma kwa waajiri ya upandishwaji madaraja pamoja na ubadilishaji wa kada ili yafanyike kwa wakati kupunguza malalamiko kwa watumishi?

Swali la pili, napongeza sana speed iliyopo ya kupandisha madaraja kwa mfumo wa mserereko hasa walimu, kwa vile kada zingine wengi wanakwenda kustaafu na kumekuwa na malalamiko mengi miongoni mwa kada zisizo za ualimu.

Je, Serikali haioni kuna haja ya kuweka speed ile ile ya kupandisha madaraja kwa mserereko kwa kada nyingine? Ahsante. (Makofi)

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza ninapokea pongezi za Serikali alizozitoa Mheshimiwa Dkt. Alice, kwa namna Serikali ilivyoshughulikia upandishaji vyeo wa watumishi wa umma hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mkakati wa mwongozo tulioutoa mwezi Aprili, 2024 kuwataka waajiri wote katika sekta ya umma walete orodha ya watumishi wale wanaostahili na wenye sifa ya kupandishwa vyeo ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hili tutalifuatilia na ninashukuru sana waajiri wengi wameweza ku-respond na kuleta hao wanaostahili kupandishwa vyeo na nitumie Bunge hili kutoa rai kwa wale ambao bado hawajatimiza ndani ya wiki moja wakamilishe ili tutakapoanza mwaka mpya wa fedha watumishi wote ukiachia walimu na ambao siyo walimu waweze kupandishwa vyeo kwa kadri ambavyo tumepanga bajeti ya takribani shilingi bilioni 207.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu speed ya kupandisha kada nyingine nikutoe shaka Mheshimiwa Dkt. Alice, haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama nilivyosema bajeti ipo na azma yake ni kwamba tutakapofika mwaka mpya wa fedha 2025/2026 kusiwe na malalamiko ya watu waliolimbikizwa madaraja, wawe tumeondoa ili tuanze ukurasa mpya katika mwaka mpya wa fedha, nakushukuru.(Makofi)