Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 490 2025-06-03

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -

Je, kwa nini Serikali isipeleke ajira kwenye ngazi ya halmashauri ili kuweka uwiano wa nafasi katika kila jimbo?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2008, Toleo la 2 Aya ya 4.2, nafasi za ajira hutolewa kwa ushindani na kwa kuzingatia sifa stahiki kwa mujibu wa Miundo ya Maendeleo ya Utumishi ya kada husika. Vilevile mgawanyo wa nafasi za ajira mpya katika utumishi wa umma huzingatia mahitaji ya watumishi yaliyoainishwa na mwajiri na kisha kuidhinishwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika ikama na bajeti kwa mwaka wa fedha husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Ofisi ya Rais, Utumishi kuidhinisha kibali cha ajira mpya, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma huendesha usaili wa kuwapata watahiniwa stahiki na kisha kuwapangia katika maeneo yenye uhitaji ili kujaza nafasi wazi kulingana na mahitaji ya mwajiri kwa mwaka husika. Kwa msingi huo nafasi za ajira mpya haziwezi kutolewa kwa uwiano sawa kwa kila jimbo, nashukuru.