Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 491 2025-06-03

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Arumeru Mashariki lina jumla ya vitongoji 330 ambapo kati ya hivyo, vitongoji 284 vimepatiwa umeme, 17 vipo katika hatua ya utekelezaji kupitia mradi wa ujazilizi na mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji Awamu ya Pili A. Vitongoji 29 zabuni imetangazwa ili kupata wakandarasi wa kutekeleza miradi kupitia mradi wa kupeleka umeme vitongojini Awamu ya Pili B.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukamilika kwa miradi hii kutawezesha vitongoji vyote vya Jimbo la Arumeru Mashariki, kufikiwa na umeme, ahsante. (Makofi)