Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na nichukue nafasi hii kwa kweli kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita na kuipongeza kwa kazi nzuri sana ambayo inafanya katika kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanakuwa nuruni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata za Mashariki mwa Jimbo langu kwa maana ya King’ori, Leguruki, Maruvango, Ngarenanyuki na Ngabobo zinapata maji kutoka msitu wa Mlima Meru lakini maji haya yana fluoride nyingi. Taasisi ya KOICA imejitolea kutuletea mitambo ya kusafisha maji haya na kuhakikisha kwamba yanakuwa free of fluoride.

Je, ni lini Serikali itatupelekea umeme wa uhakika kwenye Kitongoji cha Seneto eneo ambalo KOICA wameweka hii mitambo?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge na nikiri Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia jambo hili kwa muda sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tulishamuelekeza Meneja wa Arumeru Mashariki na tayari wameshatenga fedha kwa ajili ya mwaka wa ujao wa fedha kwa ajili ya kupeleka umeme wa uhakika katika Kitongoji hiki cha Seneto, Kata ya Leguruki kwa ajili ya kutibu fluoride na kuondoa fluoride katika maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge suala hili tunaenda kulitekeleza na mimi kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri nimkumbushe Meneja wa Arumeru Mashariki ahakikishe kuanzia mwezi wa saba jambo hili linatekelezwa ili wananchi wa Arumeru Mashariki hususan katika maeneo ambayo ameyataja Mheshimiwa Mbunge wapate maji ya uhakika ambayo yanaondolewa fluoride katika mitambo ile. (Makofi)

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 2

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi. Je, ni lini Serikali itawaunganishia umeme wananchi wa Kitongoji cha Orera katika Kijiji cha Mweka, Kata ya Kibosho Mashariki? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, katika Jimbo hili la Moshi Vijijini yupo mkandarasi ambaye anatekeleza miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji katika vile vitongoji 15 vya kila Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kitongoji hiki cha Orera ambacho Mheshimiwa Mbunge amesema na chenyewe kipo katika mradi huu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge mkandarasi ambaye anaitwa Silex Engineering yupo site anaendelea na kazi ya upimaji. Kwa hiyo, niwahakikishie wananchi hawa wa Orera wataenda kupata umeme hivi karibuni kwa sababu tayari mkandarasi yupo site. (Makofi)

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 3

MHE. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia na mimi nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ninapenda kujua; ni lini sasa watatupelekea umeme kwenye Mitaa ya Mongoroma, Chandimo na Hachwi? Hii mitaa na yenyewe ina haki ya kupata umeme tafadhali. (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsantena nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake. Ni kweli kuna mitaa ya Kondoa Mjini ambayo ilikuwa haina umeme na tulishapunguza baadhi ya mitaa imebaki hii mitaa mitatu ambayo Mheshimiwa Mbunge amesema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie kuwa tunaendelea kutenga fedha katika bajeti ya TANESCO ili kwa mwaka ujao wa fedha tuendelee kupunguza na kwenda kuweka umeme katika mitaa hii mitatu. Tutaenda kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha na bajeti ambayo imetengwa. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 4

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Jimbo la Mwibara bado lina vitongoji vingi ambavyo havina umeme. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika vitongoji hivyo? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na miradi ya vitongoji inayoendelea katika Jimbo la Mwibara pia watanufaika na mradi huu mkubwa unaokuja kupeleka umeme kwenye Vitongoji Awamu ya Pili B kwani Jimbo la Mwibara na lenyewe limetengewa vitongoji.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali itaendelea kupeleka umeme kwenye vitongoji kadri ya upatikanaji wa fedha na kwa mradi huu wataendelea kunufaika pia. (Makofi)

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Kata ya Ilula - Kijiji cha Igingilanyi, Wilaya ya Kilolo nguzo zimewekwa tangu mwezi wa 11 mwaka jana mpaka leo hii umeme haujawashwa na wananchi wanasubiri kwa hamu. Je, lini sasa umeme huo utawashwa? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninamshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake; ninalifahamu eneo lile tulipata changamoto kidogo kwa sababu eneo hili lilikuwa la ziada, lakini nimhakikishie tayari tumeshajipanga mpaka kufikia mwezi wa saba tutakuwa tumepeleka pale nyaya na kufikisha umeme katika eneo husika. Nimkumbushe Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini wamuongezee mkandarasi addendum pale ili aweze kukamilisha kazi hii ili wananchi waendelee kunufaika na upatikanaji wa umeme katika eneo hilo. (Makofi)

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 6

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika vitongoji vya Mkoa wa Simiyu ambavyo havina umeme? (Makofi)

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, tayari kuna miradi ya vitongoji inaendelea katika Mkoa wa Simiyu lakini kwa mradi wa kupeleka umeme katika Vitongoji Awamu ya Pili B na Mkoa wa Simiyu pamoja na majimbo yake yote na yenyewe yako katika mkakati. (Makofi)

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha kusambaza umeme wa REA kwenye vitongoji 37 ambavyo vipo gizani katika Jimbo la Arumeru Mashariki?

Supplementary Question 7

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwenye vitongoji 15 vya Mbunge katika Jimbo la Babati Mjini vitongoji sita line kubwa ipo mbali hivyo tukaomba TANESCO mtusogezee umeme kwenye hivyo vitongoji ili REA waendelee. Ni lini mtatupatia hizo fedha?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, baada ya kutoka hapa ninaomba nifanye mawasiliano na wenzangu ili kuweza kuona ni kwa namna gani tutaweza kusaidia katika maeneo haya sita ambayo amesema Mheshimiwa Mbunge ili na wananchi wake na wenyewe waendelee kunufaika na miradi hii ya kupeleka umeme.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge nikitoka hapa basi tutafanya mawasiliano kuona namna gani tutatafuta hizo fedha kwa ajili ya kuanza kupunguza kero hii katika maeneo ambayo ameyasema.