Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 492 2025-06-03

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa soko la zao la pareto?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali katika mwaka wa fedha 2024/2025 imetekeleza mikakati mbalimbali ili kuongeza uzalishaji wa zao la pareto nchini ikiwemo kusambaza mbegu bora kilo 890 za pareto kwa wakulima 3,500 katika maeneo ya uzalishaji na kuboresha mifumo ya upatikanaji wa soko kwa kusajili kampuni 11 za kununua na kuchakata pareto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 imepanga kuongeza uzalishaji wa pareto kufikia tani 5,000. Lengo hilo litafikiwa kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo kusambaza mbegu bora za pareto kilo 5,300 kwa wakulima; kutoa mafunzo kuhusu kanuni za kilimo bora cha zao la pareto kwa wakulima viongozi 19,000 na wakaguzi wa pareto 50; na kuratibu ujenzi wa makaushio 150 ya pareto katika Halmashauri za Makete, Ileje, Mbeya, Ludewa, Mbulu na Arusha.