Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: - Je, kuna mkakati gani wa kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa soko la zao la pareto?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana, pamoja na uzalishaji mdogo huu wa pareto nchini, lakini Tanzania inaongoza Afrika kwa uzalishaji wa zao hili la pareto. Kuna changamoto kubwa sana ya mnyororo wa thamani ya hili zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima analipwa shilingi 3,700 kwa kilo wakati yule mnunuzi akiisaga analipwa shilingi 6,000 kwa kilo na ukitengeneza ikiwa crude kwa kilo inauzwa 200,000 na refinery inauzwa shilingi 1,000,000 kwa kilo. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukiangalia huu mnyororo unaona kabisa kuwa mkakati uliopo siyo mzuri na haumsaidii sana mkulima wala kuisaidia nchi yetu. Je, ni kwa nini sasa Serikali isirudishe bodi maalum ili iweze kusimamia zao hili muhimu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa sababu tuna kiwanda cha kuzalisha viuatilifu pale Kibaha ambacho kinaweza kuzalisha viuatilifu kutumia pareto. Ni kwa nini, Serikali isiwe na mkakati maalum sasa ili zao hili liweze kutuletea viuatilifu ambavyo ni organic kutoka hapa hapa nchini? (Makofi)
 
											Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
								NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, mimi nimthibitishie tu Mheshimiwa Njeza kwamba moja ya zao ambalo sisi Serikali tunalipa kipaumbele sasa hivi ni pamoja na zao la pareto. Pia mnatambua kabisa kwamba tangu Mheshimiwa Rais ameingia madarakani ndio unaweza kuona mazao ambayo yalikuwa yamepotea sasa hivi yananyanyuka ikiwemo zao la pareto ambalo kwa sasa sisi ni wa kwanza Afrika na wa pili nafikiri duniani. 
Kwa hiyo, kuhusu bodi kwa sasa yanasimamiwa na Bodi ya Mazao Mchanganyiko, lakini ni jambo ambalo lipo katika mipango yetu kulingana na uzalishaji jinsi unavyoendelea. Kwa hiyo, jambo hilo niseme tu tunalifanyia kazi. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kufufua kiwanda kwa ajili ya kuzalisha viuatilifu na lenyewe lipo katika mipango ya Serikali. Kwa hiyo, nimwondoe shaka Mheshimiwa Mbunge katika hili. 
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved