Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 493 2025-06-03

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika Jimbo la Bagamoyo hasa katika Mradi wa JICA?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Skimu ya Bagamoyo Irrigation Development Programe (BIDP) yenye ukubwa wa hekta 100 iliendelezwa na Serikali kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kwa lengo la kufundishia wakulima katika Kijiji cha Sanzale, Kata ya Magomeni, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Skimu hiyo imeendelea kufanyiwa ukarabati na kuendelezwa na Serikali kwa awamu tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika mwaka wa fedha 2025/2026 imepanga kufanya maboresho ya miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo ili kuhakikisha inazalisha kwa tija na kuongeza ufanisi wa matumizi ya rasilimali maji. Kazi ya tathmini ya uchakavu wa miundombinu ya umwagiliaji kwa ajili ya kupata gharama halisi za ukarabati wa miundombinu hiyo inaendelea.