Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika Jimbo la Bagamoyo hasa katika Mradi wa JICA?

Supplementary Question 1

MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru pia nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; eneo la skimu ya umwagiliaji hili lina ukubwa wa hekta 100 tu kama ulivyosema, lakini wenzetu wa Magereza wana eneo kubwa sana ambalo limepakana na skimu hii. Je, Wizara yako iko tayari kwenda kuzungumza na hawa watu wa Magereza kutuongezea hili eneo ili lote liwe la skimu ya uwagiliaji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Serikali ina mpango wa kujenga mabwawa makubwa kwa ajili ya uwagiliaji na pale Bagamoyo kuna mradi mmoja ambao upo katika Wizara yako Mradi wa Bwawa la Mandela; je, ni lini Serikali sasa itaanza mpango wa kujenga bwawa hili ili liweze kusaidia umwagiliaji katika mashamba ya Bagamoyo Sugar na skimu nyinginezo katika Jimbo la Bagamoyo na Chalinze? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, mimi nimpongeze sana Mheshimiwa Mkenge, Mbunge wa Bagamoyo kwa maswali mawili ya msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, utayari wa sisi Serikali; sisi muda wote tuko tayari na tutazungumza na wenzetu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kuhakikisha jambo hili linakuwa na tija kwa pamoja. Hata hivyo, moja ya mipango tuliyonayo katika ujenzi wa miundombinu ninafikiri tutawafikia mpaka katika eneo hilo. Kwa hiyo, hilo tutalifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili; kuhusu Bwawa la Mandela ambalo amelizungumzia hapa ni kwamba Bwawa hilo ni miongoni mwa yale mabwawa 100 tunayoyafanyia tathmini sasa hivi. Kwa hiyo, lipo katika mipango yetu ya Serikali na tukishakamilisha maana yake tutalipa kipaumbele yawe yale mabwawa ya mwanzoni kwa ajili ya kuanza kujengwa. Kwa hiyo, na lenyewe lipo katika mipango yetu. (Makofi)

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika Jimbo la Bagamoyo hasa katika Mradi wa JICA?

Supplementary Question 2

MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kuniona. Ninatoa shukrani nyingi sana kwa Wizara ya Kilimo na Serikali kwa ajili ya Miradi ya Sukuma na Magulukenda.

Je, Serikali ina mpango gani kwa wananchi wa Bonde la Bupandwa, Kafunzo na Luhorongoma ili waweze kupata mradi wa umwagiliaji mwaka huu wa fedha? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimthibitishie tu Mheshimiwa Shigongo na anafahamu kwamba moja ya kazi kubwa ambayo tunafanya sisi Wizara ya Kilimo ni kumalizia tathmini katika maeneo yote ambayo ameyaainisha na baada ya hiyo tathmini maana yake tutaanza kutafuta mkandarasi ili yaanze kujengwa. Kwa hiyo, yapo katika mipango yetu ya Serikali. (Makofi)