Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Water and Irrigation Wizara ya Maji 494 2025-06-03

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO K.n.y. MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha Miradi ya Maji Kijiji cha Mangio, Mwaniko na Msangeni – Mwanga?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji Mwai-Mwaniko-Mangio uliopo Wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ukarabati wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 90,000 kila moja, ujenzi wa nyumba ya mitambo (pump house), ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 17 sanjari na ujenzi wa vituo 30 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 60% na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025 na kunufaisha wananchi wapatao 5,551 waishio kwenye Vijiji vya Mwai, Mwaniko na Mangio. (Makofi)