Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 495 2025-06-03

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatatua migogoro ya mipaka ya Hifadhi Kata ya Mputa na Mchomoro, Namtumbo?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ina jukumu la kutafsiri Matangazo ya Serikali kuhusu Mipaka ya Hifadhi na Mipaka ya Kiutawala. Katika kutekeleza jukumu hili, Wizara yangu inashirikiana na Wizara za Kisekta, ikiwemo Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia migogoro ya mipaka ya hifadhi katika Kata za Mputa na Mchomoro, Wilayani Namtumbo, Wizara itaunda timu ya wataalam inayojumuisha watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais, TAMISEMI ambayo itashirikiana na Halmashauri za Vijiji vyenye migogoro ya mipaka katika kutatua migogoro husika. Timu hiyo inatarajia kuanza kazi kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2025.