Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, lini Serikali itatatua migogoro ya mipaka ya Hifadhi Kata ya Mputa na Mchomoro, Namtumbo?

Supplementary Question 1

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, kutokana na swali la Mheshimiwa Vita Kawawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali na kwa kuwa changamoto ile imekuwa ni kubwa; majibu yanasema kuna timu ambayo itakwenda kushughulikia changamoto ile. Ninataka kufahamu, je, ni lini hasa watakwenda kutatua changamoto hiyo?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, ni kwamba kabla ya mwisho wa mwezi huu wa sita tutakuwa tumepeleka timu ambayo itakwenda kupitia maeneo haya. Kusema ni lini hasa kwa sababu ni muundo wa timu kutoka karibu sekta tatu, Wizara yetu, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; mawasiliano yanaendelea ili kuandaa hii timu iweze kwenda eneo hilo haraka zaidi.

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, lini Serikali itatatua migogoro ya mipaka ya Hifadhi Kata ya Mputa na Mchomoro, Namtumbo?

Supplementary Question 2

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, kumekuwepo na mgogoro kati ya wananchi wetu wa Wilaya ya Arumeru na Longido katika Vijiji vya Engutukoiti na Engikareti. Mgogoro huu umechukuwa muda mrefu sana na tumekuwa tukifuatilia Wizarani mara kwa mara.

Sasa nataka kufahamu, ni lini Serikali kwa maana ya kupitia Wizara ya Ardhi, itakwenda kuhitimisha mgogoro huu ili wananchi waweze kuishi kwa amani na utulivu kwa sababu hata jana wameongea kwenye ITV na kuleta mtafaruku mkubwa.

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mgogoro wa Arumeru na Longido ni mipaka ya kiutawala. Tumemuelekeza Kamishna wetu wa Mkoa wa Arusha aende kwenye eneo hilo la mgogoro ili kubainisha hasa nini chanzo cha mgogoro kwa sababu mipaka hii imekwishawekwa siku nyingi na kumekuwepo na utulivu wa miaka mingi katika eneo hili, lakini sasa tukajue kisa hasa ni nini. Kwa hiyo, naendelea kumuelekeza Kamishna wa Ardhi, Mkoa wa Arusha, aende haraka sana na kuleta taarifa Wizarani ili tuone namna nzuri ya kwenda kulitatua.