Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 496 2025-06-03

Name

Soud Mohammed Jumah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Donge

Primary Question

MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuweka huduma za afya bure kama ilivyo katika elimu ya msingi na sekondari?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya kwa wananchi wasio na uwezo. Tangu mwaka 1995 Serikali imekuwa ikitekeleza Sera ya Msamaha wa Gharama za Matibabu kwa Wananchi Wasio na Uwezo. Hata hivyo, kutokana na changamoto ambazo zimeendelea kujitokeza katika utekelezaji, Serikali iko katika hatua za utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Sheria hiyo itatoa fursa kwa watu wasio na uwezo kugharamiwa bima ya afya na Serikali ili kuwawezesha kupata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.