Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Soud Mohammed Jumah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Donge
Primary Question
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuweka huduma za afya bure kama ilivyo katika elimu ya msingi na sekondari?
Supplementary Question 1
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Pia namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza; kama unavyojua kwamba Tanzania ni nchi ya ujamaa na misingi mikubwa ya ujamaa ni kutoa huduma zile muhimu katika hali ya usawa na haki. Sasa je, Mheshimiwa Waziri hauoni haja ya kuja na mpango maalum wa dharura ili kuweza kusaidia kuimarisha huduma hizi za afya kwa wale wenye vipato vya chini na vipato vya kati, ili wasitwezwe utu wao na kuweza kudhalilika wakienda hospitali? 
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali namba mbili; kwa kuwa bima ya afya ndiyo ipo katika utaratibu na inaweza ikachelewa kidogo, sasa je, hatuoni haja ya kuja na mpango wa dharura, tukatenga fedha maalum katika bajeti ya kila mwaka ili kusaidia hao wenye mazingira magumu na wananchi ambao wanashindwa kuweza kukimu hizi dharura za kiafya katika huduma zao? 
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
								NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naanza kwa kumpongeza Mbunge mwenzangu kwa namna ambavyo kwa kweli, ameliona hili swali ambalo ni nyeti na Wabunge wengi wamekuwa wakilisemea. Namhakikishia tu kitu kimoja, ujamaa unaanzia kwenye familia, lakini ni kweli hata sisi tunapopanga mipango ile mizuri ya kijamaa ndani ya familia wakati wote tunaweza tukawa tumetimiza 60%/70% ya malengo ambayo tulikuwa tumejipangia. Hata hivyo, kwenye eneo hili sasa ambalo tunalizungumzia nimewahi kusema hapa kwa miaka mitatu iliyopita, mwaka 2022 tulifanya uchunguzi na kupiga mahesabu, tukakuta kwenye eneo hili tu la kusaidia watu wasioweza kulipa malipo Serikali ilitumia shilingi bilioni 667. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwa wanawake na watoto utaona kwa mwaka 2024 tu, Serikali imetumia shilingi bilioni 157 kusaidia. Ni kweli kwamba kinachohitajika ili kuwahudumia wote ni zaidi ya shilingi bilioni 227 ambazo kwa wakati huo, kama unavyojua Mbunge mwaka huu ulitupitishia shilingi bilioni 200 kwa ajili ya dawa na vifaatiba. Kwa hiyo, nakuhakikishia kuna mifumo ya kufanya ili kuhakikisha hili unalotaka litekelezwe. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, tunaanza kwa Mtendaji wa Kata kupata barua. Anapokwenda na ile barua, itaheshimika na atatibiwa bila matatizo. 
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved