Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 38 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 497 2025-06-03

Name

Condester Michael Sichalwe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Momba

Primary Question

MHE. CONDESTER M. SICHALWE Aliuliza: -

Je, lini Serikali itavitambua vivutio vilivyopo Jimbo la Momba kama vile Nyayo za Mtu wa Kale, Nkanyama, Maporomoko ya Mfuso na Yala (Mpona)?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII Alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara ilitekeleza zoezi la kutambua vivutio vya utalii katika Wilaya ya Momba kwa lengo la kuviendeleza na kuvitumia kama bidhaa za utalii. Miongoni mwa vivutio vilivyobainishwa ni Nyayo za Mtu wa Kale, Nkanyama, Maporomoko ya Mfuso na Yala (Mpona) na Kimondo cha Ivuna. Baada ya kuvibaini vivutio hivyo, zoezi linalofuata ni kufanya tathmini ya vivutio vilivyobainishwa ili kupata vivutio ambavyo viko karibu na miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuvipa kipaumbele katika uendelezaji kwa kushirikiana na halmashauri husika na wadau wa sekta binafsi, ili kupata matokeo ya haraka.