Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 30 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 378 | 2025-05-22 | 
 
									Name
Latifa Khamis Juwakali
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuliza:-
Je, kuna mkakati gani wa kuwalinda Wanafunzi Shuleni?
					
 
									Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
						NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, usalama wa wanafunzi ni kipaumbele cha Serikali ambapo mikakati mbalimbali imekuwa ikitekelezwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa katika mazingira salama shuleni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya mikakati inayotumika kuwalinda wanafunzi ni pamoja na kampeni za kupinga ukatili wa kijinsia kuanzia nyumbani, njiani na shuleni kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama; mafunzo kuhusu shule salama kwa wadau muhimu wa ulinzi na usalama wa wanafunzi, ambapo mwaka wa fedha 2024/2025 yameendeshwa mafunzo kwa Walimu 7,451 wa ushauri na unasihi, Wakuu wa Shule za Msingi 17,817, Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya kata 900, Wenyeviti wa Kamati za Shule 1,980 na Wenyeviti wa Bodi za Shule 580. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati mingine ni kuanzisha Dawati la Ulinzi na Usalama wa Mtoto. Aidha, katika ngazi za vijiji na mitaa yameanzishwa mabaraza ya watoto yanayojumuisha wanafunzi wa msingi na sekondari na watoto waliopo kwenye mfumo usio rasmi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kufanya tathmini ya kina kuhusu changamoto zinazowakabili wanafunzi shuleni, njiani na nyumbani ili kuboresha mikakati ya kuzitatua.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved