Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 30 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 379 2025-05-22

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:-

Je, kwa nini Serikali haiwaajiri wahitimu wenye diploma kuwa Watendaji wa Vijiji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ajira za watendaji wa vijiji katika utumishi wa umma hufanyika kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa katika Muundo wa Utumishi wa Kada za Watendaji wa Vijiji/Mitaa uliotolewa na Serikali kupitia Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na.1 wa Mwaka 2013.

Mheshimiwa Spika, muundo huo umeainisha watendaji wa vijiji/mtaa wanaoajiriwa katika utumishi wa umma wanatakiwa kuwa na kiwango cha elimu ya kidato cha nne au sita waliohitimu mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika moja ya fani zifuatazo; utawala, sheria, elimu ya jamii, usimamizi wa fedha, maendeleo ya jamii na sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo) au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, kutokana na masharti hayo, wahitimu wa mafunzo ya Stashahada (Diploma) katika fani tajwa hawawezi kuajiriwa kwenye utumishi wa umma katika nafasi ya mtendaji wa kijiji/mtaa kwa kuwa sifa hiyo haijatajwa katika muundo husika. Hata hivyo, wahitimu wenye sifa hizo wanaweza kuajiriwa katika utumishi wa umma katika kada nyingine zinazotaja sifa hiyo kama sifa ya kuajiriwa. Ahsante.