Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:- Je, kwa nini Serikali haiwaajiri wahitimu wenye diploma kuwa Watendaji wa Vijiji?

Supplementary Question 1

MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni taaluma zipi ambazo wanaweza kuajiriwa ili nao waweze kupata haki ya kuajiriwa baada ya kuwa wamepata mafunzo mbalimbali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ninataka nijue; tumekuwa na upungufu wa watendaji katika vijiji na kata na tumekuwa tukichukua muda mrefu sana kujaza nafasi hizi na imeathiri sana utendaji wa Serikali kwenye maeneo yetu. Je, Serikali ina mpango gani wa muda mrefu wa kuhakikisha kwamba nafasi hizo zinajazwa na kuondoa gaps ambazo zipo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimejibu kwenye majibu ya msingi, kwamba ajira za watendaji wa vijiji na mitaa zimeainishwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa Mwaka 2013; na kwamba wenye sifa hizo ni wale waaliohitimu kidato cha nne au kidato cha sita na kupata certificate katika maeneo ya utawala, sheria, elimu ya jamii, usimamizi wa fedha, maendeleo ya jamii, sayansi ya sanaa kutoka Chuo cha Hombolo au chuo kingine chochote ambacho kinatambuliwa na Serikali. Kwa hiyo, hawa ndiyo wenye sifa za kuajiriwa kama watendaji wa vijiji au mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wenye diploma wana nafasi kwa maana ya sifa katika ajira/nafasi nyingine, lakini si watendaji wa vijiji au mitaa. Wameendelea kuajiriwa katika nafasi mbalimbali kwa nafasi hiyo ya diploma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kuhusiana na watendaji wa vijiji; ni kweli kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya maeneo; kwamba kuna vijiji vinakosa watendaji wa vijiji. Hata hivyo, Serikali imeendelea kufanya tathmini mara kwa mara na kutambua vijiji ambavyo havina watendaji na kuendelea kuwaajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda ambao unapita unatokana na taratibu zile za ajira ambazo zinachukua muda kidogo. Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba kila mahali ambapo tunakuwa hatuna mtendaji wa kijiji au mtaa, basi anapatikana mapema kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo.