Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 30 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 380 2025-05-22

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:-

Je, lini Serikali Itaanza Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mpalinga – Bahi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetenga fedha ya nyongeza shilingi bilioni 53.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya kwenye kata 214 za kimkakati. Awamu ya kwanza inaanza na ujenzi wa vituo 120 ambapo shilingi bilioni 30 zimetengwa.

Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri ya Bahi shilingi milioni 250 zitapelekwa awamu ya pili katika Kata ya Mtitaa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), choo cha nje, kichomea taka na shimo la kutupia kondo la nyuma.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika kata za kimkakati kote nchini ikiwemo Kata ya Mpalinga katika Halmashauri ya Bahi.