Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Kenneth Ernest Nollo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bahi
Primary Question
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali Itaanza Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mpalinga – Bahi?
Supplementary Question 1
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishukuru Serikali kwa dhati kwa namna ambavyo imeweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mtitaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Serikali imejenga Kituo cha Afya Babayu, lakini hadi sasa zile huduma za kituo cha afya hazijaanza kutolewa, hususani upasuaji, je, ni lini zitaanza?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; ni kwamba, Serikali ilianza ujenzi wa Kituo cha Afya pale Kata ya Chifutuka na kilishakamilika lakini jengo la OPD halikujengwa.  Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Chifutuka kwenye OPD ili wananchi waanze kupata huduma kamilifu? 
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Ernest Kenneth Nollo, kwa namna ambavyo ameendelea kuwasemea na kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Bahi. Vilevile ninafahamu kwamba anafuatilia sana kuhusiana na kukiwezesha Kituo cha Afya cha Babayu kuanza kutoa huduma. Mimi na yeye tulifanya ziara katika kituo kile cha afya na tuliona majengo yakiwa hatua za mwisho za ukamilisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa jengo la upasuaji la Kituo cha Afya cha Babayu limekamilika, lakini taratibu za kuanza huduma ya upasuaji ziko mwishoni. Ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bahi; kwa sababu Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alikwishapeleka fedha, milioni 500 na majengo yamejengwa likiwepo jengo la upasuaji na limeshakamilika. Vilevile, Mheshimiwa Rais amepeleka fedha za vifaa tiba vyote kwa ajili ya upasuaji. Kwa hiyo ninaomba nitoe maelekezo haya kwa mkurugenzi kwamba tunawapa mwezi mmoja. Ifikapo tarehe 30 Juni jengo la upasuaji katika kituo hiki cha afya lianze kutoa huduma za upasuaji kwa wananchi. Ahsante. 
							
 
											Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali Itaanza Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mpalinga – Bahi?
Supplementary Question 2
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Kituo cha Afya cha Ngongoele kilipata fedha milioni 250 zile za matokeo makubwa sasa, mradi ambao ulishakwisha. Je, Serikali ina mpango upi wa kutupatia fedha, milioni 200 nyingine ili kukamilisha kituo kile?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kujenga vituo vya afya na kuvikamilisha kwa awamu. Tunafahamu kwamba Kituo cha afya cha Ngongoele katika Jimbo la Liwale bado hakijakamilika. Serikali ilikwishapeleka fedha kwa awamu ya kwanza. Nimhakikishie kwamba tutaendelea na awamu ya pili, ambapo tutapeleka fedha kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kituo hicho kinajengwa na kukamilika ili kianze kutoa huduma kwa wananchi ambazo zina ngazi ya kituo cha afya.
 
											Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza:- Je, lini Serikali Itaanza Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mpalinga – Bahi?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Je, ni lini Serikali itamalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Mafisa katika Manispaa ya Morogoro? Ahsante sana.
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Mafisa katika Manispaa ya Morogoro ni moja ya vituo vya afya ambavyo vina upungufu wa majengo. Tayari Serikali ilikwishaainisha majengo yanayopungua na tumekwishaweka kwenye mpango wa bajeti kupitia Mfuko wa Benki ya Dunia. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, fedha zitapelekwa kwa ajili ya ukamilishaji wa kituo hicho cha afya.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved