Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 30 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 382 | 2025-05-22 | 
 
									Name
Michael Constantino Mwakamo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
						MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-  
Je, Serikali haioni ni muda muafaka kuchimba visima vya maji kwenye Taasisi za Umma kama shule, zahanati na hospitali zote nchini?
					
 
									Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
						NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza inapatikana katika maeneo yote ikiwemo taasisi za umma kama vile shule na vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Serikali huzingatia uwepo wa taasisi hizo wakati wa usanifu wa miradi ya maji na hivyo kuhakikisha mahitaji yake yanajumuishwa. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali kupitia miradi mbalimbali iliyotekelezwa imefikisha huduma ya maji safi na salama kwa taasisi za umma 31,130 ambapo kati ya hizo, shule za msingi na sekondari ni 25,820 wakati Vituo vya kutolea huduma za afya ni 5,310.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuzingatia mahitaji ya maji kwa taasisi zote za umma nchini kupitia miradi inayoendelea na inayotarajiwa kujengwa pamoja na kufikisha huduma ya maji kadri itakavyohitajika.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved